Course Content
Utangulizi
Kupunguza uzito na kitambi ni rahisi sana japo nafahamu kuna wengine wanahangaika. Hiyo inatokana na kuwa wanatumia njia ambazo sio sahihi. Pamoja na kuwa katika program hii nimekufundisha pia kwa ufupi jinsi ya kupungua lakini sana ninalenga kukusaidia usiongezeke tena. Hapo ndio panahitaji uelewe zaidi.
0/1
Wiki 1: Detox & Mwanzo Mpya
Hapa tunaweka msingi wa mabadiliko ya mwili na akili kwa kuondoa mazoea na sumu za zamani, kuanzisha mpangilio bora wa kula, na kujenga muunganiko wa ndani na safari ya kupunguza uzito kwa njia ya asili na endelevu.
0/6
Module 2: Tabia Mpya & Saikolojia ya Kupungua Uzito
Utajifunza jinsi ya kujenga misingi ya kitabia na kiakili kwa kutumia mikakati ya kisaikolojia ili kuwezesha mabadiliko ya kudumu. Hapa utjenga ubongo mpya – kwa vitendo vidogo vinavyoweza kuleta mabadiliko makubwa kwa muda mrefu.
Module 3: Viungo vya Uponyaji – Badilisha Sahani Yako, Badilika
Fahamu na anza kutumia viungo vya asili vyenye nguvu ya tiba kila siku ili kusaidia kupunguza uzito, kupunguza uvimbe mwilini, kuboresha mmeng’enyo, na kuimarisha afya kwa ujumla bila kutumia virutubisho vya viwandani.
Module 4: Shiba Kifalme – Bila Kuongeza Uzito
Utajifunza kula kwa ujanja na kuridhika bila kula kupita kiasi. Unapata ujazo mkubwa tumboni kwa kutumia vyakula vyenye calorie density ya chini, lakini vyenye virutubisho vingi – unashiba bila kuongezeka uzito.
Module 5: Vinywaji vya Upinyaji na Upunguaji
“Unachokunywa kinaweza kukuletea njaa au kukupatia afya – chagua busara.” Katika mwezi huu, tutajifunza jinsi ya kutumia vinywaji kama sehemu ya mkakati wa kudhibiti uzito kwa kudhibiti njaa, kuongeza metabolism, na kusaidia detox asilia ya mwili. ________________________________________ 🎯 Malengo ya Mwezi: • Kutofautisha kati ya vinywaji vinavyosaidia afya na vinavyoharibu • Kujenga tabia ya kunywa maji kwa ufanisi kila siku • Kujifunza faida za green tea, apple cider vinegar na tiba ya maji moto asubuhi • Kuelewa athari za vinywaji vyenye kalori nyingi, sukari na kafeini kupita kiasi
Module 6: Deflour & Nafaka Kamili – Rudisha Uasili wa Kula
Utajifunza jinsi ya kuondoa unga uliokobolewa (refined flour) na bidhaa zake kwenye lishe, kuanzisha nafaka kamili, mikunde, na vyakula vyenye glycemic index ya chini. Hii husaidia kudhibiti sukari kwenye damu, kuongeza nishati na kushiba kwa muda mrefu – silaha muhimu dhidi ya kitambi na njaa ya mara kwa mara.
Module 7: Mazoezi kwa Ajili ya Uzito Bora – Siyo Gym Tu, Ni Mtindo wa Maisha
Kujenga tabia ya kutembea, kufanya mazoezi mepesi lakini yenye tija, kuongeza harakati ndogondogo kila siku ili kuamsha mwili, kuchoma mafuta, na kuimarisha afya bila kutumia vifaa ghali au uwanja wa mazoezi.
Module 8: Superfoods kwa Uzito Bora na Kinga Imara
Utajifunza jinsi ya kuimarisha afya ya mwili kwa kutumia vyakula vyenye uwezo wa kipekee wa kupunguza uzito, kulisha mwili vizuri, na kusaidia kinga asilia – bila virutubisho vya viwandani au gharama kubwa.
Module 9: Kweli Kuhusu Nyama, Samaki, Mayai & Maziwa
Hapa utaweka msingi wa maarifa sahihi kuhusu protini kutoka kwa wanyama, madhara yake kwa afya na uzito, na kupata mbadala wa asili unaoridhisha, unaoshibisha, na unaotibu.
0/1
Module 10: Mapishi & Ratiba ya Chakula ya Mwezi Mzima
Utajifunza kupanga, kuandaa, na kufurahia milo ya kila siku inayojenga afya, ikizingatia mlo kamili wa mimea, upangaji wa ratiba ya kula, na kudhibiti mazingira ya kula kwa mafanikio ya muda mrefu.
Module 11: Kujipongeza & Kujiamini (Spiritual & Emotional Alignment)
Kujenga ujasiri wa ndani, kusherehekea mafanikio, na kuunganisha safari ya kupungua uzito na ustawi wa kiroho, kihisia, na kimahusiano. Huu ni wakati wa kujitazama kwa upendo na kukuza imani kuwa una uwezo wa kuendelea bila kurudi nyuma.
Module 12: Tathmini, Maboresho & Mahafali
Kusanya mafanikio yote ya miezi 11, kufanya tathmini ya kina ya mabadiliko ya mwili, akili na tabia, kurekebisha maeneo yenye changamoto, na kuhitimisha safari kwa sherehe ya mafanikio (graduation) inayoweka msingi wa maisha mapya ya kudumu.
Mahafali na Hitimisho
Pungua Milele Coaching
0% Complete
Share