Kuhusu Dr Nature

Dr Nature ni jina la utambulisho wangu wa kitaaluma kama Kocha wa Maisha ya Kiafya, linalowakilisha falsafa yangu ya uponyaji kwa njia ya asili.

Mimi ni Dkt. Yusufu Mohamed Filemon, daktari wa tiba ya kawaida (MD) niliyejifunza pia tiba ya mtindo bora wa maisha (lifestyle medicine) na naturopathy.

Kama Healthy Lifestyle Coach

Kazi yangu ni kukuongoza hatua kwa hatua katika maeneo kama lishe sahihi, mazoezi yanayokufaa, usingizi bora, kudhibiti msongo wa mawazo, na kuacha tabia zinazodhuru afya. 

Lengo langu si tu kukusaidia kupunguza dalili, bali kukusaidia kubadilisha maisha yako kwa njia ya asili, salama na ya kudumu.

Share