Jinsi ya Kutibu Crohn’s Disease Kwa Chakula

Ugonjwa wa Crohn ni ugonjwa wa tumbo ambao huleta
– Maumivu ya tumbo
– Kuharisha
– kupungua uzito
– damu kwenye kinyesi
Huu ni ugonjwa sugu unaweza kumletea mgonjwa mateso makubwa. Lakini kuna habari njema – tafiti zinaonyesha kuwa lishe sahihi inaweza kusaidia sana katika kupunguza dalili, na hata kupelekea uponyaji wa kudumu.
Watu wengi wenye Crohn’s Disease huwa wanaambiwa wale chakula laini au kuepuka baadhi ya vyakula. Lakini utafiti mpya unaonyesha kuwa badala ya kuepuka tu, kuna nguvu kubwa katika kuchagua vyakula sahihi—hasa vyenye virutubisho vingi kutoka kwenye mimea.
Tafiti zinaonyesha kuwa watu waliobadili lishe yao na kula mlo wa mimea pekee walipata nafuu kubwa. Wengine walikuwa na upasuaji uliopangwa kufanywa, lakini baada ya kubadili lishe, upasuaji haukuhitajika tena. Pia, hawakuwa na dalili kwa muda mrefu—mpaka miaka kadhaa bila kurudia kwa ugonjwa.
Lishe ya mimea ina virutubisho vingi vinavyopambana na mioto mwilini (inflammation). Hii husaidia kutuliza ugonjwa. Pia, vyakula vya mimea huimarisha bakteria wazuri kwenye utumbo ambao hulinda afya ya njia ya chakula.
VYAKULA VYA KUEPUKA
• Nyama (haswa nyekundu na iliyosindikwa)
• Maziwa
• Mayai
• Vyakula vyenye mafuta mengi
• Fast foods kama biskuti, chips, soda, n.k.
VYAKULA VYA KULA ZAIDI
• Matunda kama mapapai, ndizi, maembe, na matikiti
• Mboga za majani kama mchicha, matembele, na sukuma wiki
• Maharage, dengu, kunde na njegere
• Ulezi, mtama, brown rice
• Mbegu kama karanga, alizeti, ufuta (kwa kiasi)
0 0 votes
Article Rating
Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Share