Jinsi ya Kutumia “MAJI” Kwa Usahihi Kuchoma Mafuta (Punguza Uzito na Kitambi) Milele

….”Gundua Namna Sahihi Ya Kutumia Maji Kama Silaha Mojawapo Ya kupambana na uzito mkubwa Na Kitambi…..”

Kunywa maji ya kutosha kila siku kunasaidia Kuchoma mafuta ya ziada mwilini. Na pia ni namna nzuri unayoweza kutumia kwa muda mrefu kutunza uzito wako kiafya

Kivipi Maji Yanasaidia?

1. Yanapunguza matumizi ya vinywaji vibaya

Ukinywa maji mengi kwa siku yanakupunguzia kiu na nafasi ya kunywa vinywaji vibaya kama;

  • Soda
  • Energy drink
  • Pombe N.k

2. Yanakusaidia Kula Vizuri

Tafiti zinaonesha wanaokunywa maji ya kitosha wanakula zaidi;

  • Matunda
  • mbogamboga Na
  • Mbegu nzima

Na wanakula kwa uchache vyakula ambavyo sio hai tofauti na ambao hawanywi maji

Hata wewe fikiria siku ambazo hujanywa maji vyakula unavyopendelea..

3. Maji Yanapunguza 'Angiotensin'

Angiotensin ni kemikali inayozalishwa na mwili na kazi yake mojawapo ni:

  • Kuongeza kiu ya majji
  • Kuifanya mishipa ya damu iwe mwembamba na hivyo kupandisha presha
  • Kuhamasisha mwili kutunza mafuta

Ukinywa maji ya kutosha kila siku unasaidia kupunguza hii kemikali na hivyo mafuta yanachomwa zaidi kuliko kutunzwa

4. Maji Yanaongeza kasi ya shughuli za mwili 'Metabolism'

Shughuli za mwili ikiwemo ‘Kuchoma mafuta’ zinahitaji maji ya kutosha

Ukinywa maji kunasaidia mwili uweze kufanya kazi zake ipasavyo.

Maji Kiasi Gani Yanatosha Kuchoma Mafuta?

Sio wazo zuri kunywa maji kulingana na uzito kwa sababu kadri unavyokuwa kibonge uwezo wa figo zako unapungua..

Hata hivyo kanuni inayokubalika kuwa salama ni kunywa maji kulingana na umri..

Kwa watu wazima Miaka 19+

  • Wanawake: Vikombe 9 (sawa na lita 2 na robo)
  • Wanaume: Vikombe 13 (sawa na lita 3 na robo)

Hicho ni kiwango cha chini.. Unaweza ukanywa zaidi kidogo kidogo kwa siku nzima

…”Usinywe maji meeengi kwa mara moja”..

Kama unaumwa

  • Figo
  • ⁠Moyo

Ni vema ukafuata maelekezo ya daktari wako!

Ikiwa utakunywa kinywaji kingine kizuri kiafya kama Chai ya viungo ni mojawapo ya kiasi hicho..

Kama umekunywa kikombe kimoja cha chai utaihesabu kwemye kiasi hicho cha maji..

⚠Lakini usihesabu ukinywa 

  • Pombe
  • soda, energy drink
  • kahawa

N.k

..“Muda mzuri wa kunywa maji ni asubuhi kabla hujala..”

⚠Na joto la maji halina mchango kwenye kuchoma mafuta

Sio kwamba ukinywa ya moto ndio mafuta yanaungua😂😂 HAPANA!

Kunywa ya joto la kawaida unalopenda kulingana na hali ya hewa sio baridi sana wala moto sana ukaharibu koo!

2 1 vote
Article Rating
Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Share
Scroll to Top