Maziwa Yanafaa Katika Kupunguza Uzito & Kitambi?

Jibu ni NDIO na HAPANA..!

Jibu hasa linategemea ni aina gani ya maziwa yanayotumika.

Ukisikia neno “MAZIWA”.. Kinachokuja kichwani mwako ni ‘maziwa ya ng’ombe’.

Unafahamu kuna maziwa ya aina nyingi sana, tofuati na hayo ya ng’ombe?

Hapo najua umekumbuka maziwa ya mbuzi na ngamia.. hahaha! ni sawa lakini.

Hata hivyo..

Kuna maziwa mengine ambayo hayatokani kabisa na wanyama. Na haya ni maziwa ya ‘mimea’. Unaweza ukawa bado hujaelewa ila nitakufafanulia vizuri.

Kwahiyo..

Hapo Utakuwa umeanza kupata picha kuwa kuna maziwa aina nyingi ambayo tunaweza kuyagawanya katika makundi mawili; maziwa ya wanyama na maziwa ya mimea.

Tofauti ya Maziwa ya Wanyama na Maziwa ya Mimea

Iko wazi kwamba maziwa ya wanyama yametokana na wanyama kama ng’ombe, mbuzi, ngamia n.k na maziwa ya mimea yametokana na mimea kama vile karanga, korosho, makadamia, almondi, ufuta, nazi, soya nk.

Lakini hasa nataka nikuoneshe tofauti ambazo zipo kati ya haya maziwa zinazohusiana na mwili kulundika mafuta.

Mafuta

Kuna makundi matatu ya mafuta; saturated, unsaturated na transfat. Mafuta aina ya saturated ni mafuta ambayo ni mabaya sana kwa sababu yanasababisha mioto ‘inflammation’ na kusababisha uzito mkuwa.

Aina hii ya mafuta inapatikana kwenye maziwa ya wanyama, siagi, jibini, aina zote za nyama na baadhi ya mafuta ya mimea. Kwahiyo unaponywa maziwa ya wanyama sio tu kwamba haikusaidii kupunguza uzito ila inakuongezea uzito na kitambi.

Maziwa ya mimea kwa sehemu kubwa yanakuwa na aina ya mafuta aina ya unsaturated ambayo ni mazuri na baadhi ya maziwa ya mimiea yanakuwa na saturated fat kama maziwa ya nazi. Hata hivyo wingi wa virutubisho vilivyomo kwenye maziwa ya mimea kunaleta matokeo mazuri kwa ujumla.

Vizima Moto ‘Antioxidants’

Unafahamu vile ukiwa na uzito mkubwa huwezi ukaacha kula.. yaani kila wakati ni wewe na msosi. Hamu ya chakula iko juu na kila wakati unataka kula. Hii ni kwa sababu mawasiliano ya mwili yameharibika na hivyo mwili hauwezi kutawala hamu ya kula.

Kinachoharibu uwezo wa mwili ni mioto ‘inflammation’ ambayo inawaka hadi kwenye ubongo. Matokeo yake ubongo unashindwa kufanya kazi vizuri.

Maziwa ya wanyama yanasababisha mioto ‘inflammation’ kwa sababu ya mafuta yake mabaya na pia hayana vizima moto kabisa..

Maziwa ya mimea hayasababishi mioto na pia yana wingi wa virutubisho ambavyo vinazima mioto ‘antiinflammatory’. Unapokunywa maziwa ya wanyama sio tu kwamba unajichelewesha kupungua lakini unajiongezea uzito na kitambi.

Kukaba Virutubisho

Unafahamu mtu akinywa sumu kwa bahati mbaya anapewa maziwa… umewahi kufikiria maziwa yanakusaidiaje sumu isikudhuru sana?

Protini za maziwa huwa zinaungana na viambata vya sumu na kuvishikilia ili visiingie kwenye mfumo wa damu. Inatokea hivyo hata kwenye virutubisho unavyokula pamoja na au muda mfupi kabla au baada ya kunywa maziwa ya wanyama.

Baadhi ya virutubisho muhimu kama madini ya chuma na viondoa sumu ‘antioxidants’ na vizima moto ‘antiinflammatory’ huwa vinashikiliwa na maziwa na huvipati kabisa.

Sasa ona hasara…!

Maziwa ya wanayama yenyewe hayana viondoa sumu wala vizima moto halafu yanakaba virutubisho hivyo visiingie kwenye mwili.. unakuwa umepata hasara.

Kumbuka kuwa tunapokuwa tunafanya program ya ‘Permanent Weightloss’ tunalenga kupunguza uzito kiafya katika namna ambayo itakuwa endelevu na yenye kuleta faida zaidi katika afya zetu kwa ujumla.

Hivyo, hata kama maziwa ya wanyama yangekuwa yanasaidia kupunguza uzito (yanafanya kinyume chake) bado yasingetufaa katika program yetu kwa sababu yanamadhara mengi kiafya kuliko faida zinazotangazwa.

Iwe maziwa fresh au mgando yote ni yale yale. Hata kama unatengeneza milk shake au smoothie unaweka maziwa ya wanyama, hata zile faida za matunda uliyoweka hutapata kwa kiasi kama ambavyo usingeweka yale maziwa.

Mbadala

Mbadala wa maziwa ya wanyama ni maziwa ya mimea. Mfano wa mimea/mbegu unazoweza kutengeneza mziwa yake ni soya, korosho, nazi, ufuta, makadamia, karanga nk. Jifunze jinsi ya kutengeneza na uyafurahie.

Sio tu kwamba yatakusaidia katika safari yako ya kuchoma mafuta lakini pia yatakusaidia kutunza afya yako na kutunza uzito wako ubakie kuwa mzuri milele.

Ninaamini kuwa unajua kutengeneza maziwa ya nazi ‘tui la nazi’ wacha nikuoneshe jinsi ya kutengeneza maziwa ya soya. Ni mazuri sana kwa wingi wa virutubisho vyake.

Jinsi ya Kutengeneza Maziwa ya Soya

Maziwa ya soya

Mahitaji:

  • Maharage ya soya yaliyolowekwa masaa 8-12 kikombe 1
  • Maji Vikombe 4

Maelekezo:

Hakikisha maharage ya soya uliyolowekwa unayotoa maganda kwa kupekecha kati ya viganja vyako. Sio lazima yote yatoke (inaweza kuwa ngumu sana) lakini hakikisha kwa sehemu kubwa umeyatoa maganda. Njia rahisi ni kununua soya ambayo tayari imekobolewa ndio unaloweka.

Weka kikombe 1 cha maharage ya soya kwenye blenda pamoja na maji kikombe 1 au 2. Saga hadi iwe laini kabisa kabla ya kuongeza maji yaliyobaki. Saga hadi upate ulaini wa maziwa,

Chuja kwa kutumia kitambaa safi kisha chemsha.

Unapochemsha tumia moto kiasi na uwe unakorogakoroga ili kuzuia yasiungulie kwa chini wala yasimwagike. Chemsha kwa dakika 20 hadi 30 hadi harufu ya maharage ya soya iishe.

Tayari maziwa yako yapo tayari kwa matumizi.

Matumizi:

Unaweza ukayatumia maziwa ya soya katika namna zote na mapishi yote unayotumia maziwa ya wanyama. Yanafaa hata kwa watoto wadogo kuanzia miezi 6.

Unaweza Ukayawekea viungo vingine vyovyote unavyotaka ili kuyanogesha.

Utunzaji:

Yatunze kwenye friji na unaweza pia ukayagandisha kutengeneza mtindi au yogurt.

4.3 4 votes
Article Rating
Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Anonymous
Anonymous
26 May 2023 12:11

Asante sana

Share
Scroll to Top