Hi..
Leo ni siku ya kuelekezana moja mbili za kuimarisha ndoa zetu. Maana bila unyumba ndoa ipo mashakani..
Sio tu ndio kuwa mashakani inaleta msongo mkubwa wa mawazo inaweza ikapelekea mwanaume kushindwa kufanya kazi zako na stress kuwa kubwa zaidi..
Wengine wanafikia hata kuwa na mawazo ya kujiua kwa sababu ya titizo hilo kwa sababu vile unajisia huna thamani tena..
Kabla sijazama kwenye upungufu, fahamu haya kuhusiana na tendo la ndoa
Hoja #1
Limekusudiwa kufanyika kati ya mwanaume na wanamke tu.. na sio mwanaume na mwanaume au mwanamke na wanamke. Ngono ya jinsi moja au ngono ya kujiridhisha mwenyewe kwa kujichua, midoli au mashine ni uchafu na laana kubwa..
Na sio hivyo tu.. kati ya mwanaume na mwanamke ni uchafu kwenda kinyume na maumbile ya asili yaani uke na ume na sio vinginevyo..
Sio mimi niliyesema..
Rejea Warumi 1:26,27
“Hivyo Mungu aliwaacha wafuate tamaa zao za aibu, hata wanawake wakabadili matumizi ya asili kwa matumizi yasiyo ya asili; Warumi wanaume nao vivyo hivyo waliyaacha matumizi ya mke, ya asili, wakawakiana tamaa, wanaume wakiyatenda yasiyopasa, wakapata nafsini mwao malipo ya upotevu wao yaliyo haki yao.
Hoja #2
Tendo la ndoa limeumbwa kwa binadamu kwa ajili ya wanandoa.. ndio maana likaitwa tendo la ndoa na sio tendo la urafiki wala la uchumba
‘Ngono kati ya wasiowanandoa ni uzinzi au uasherati’
Sitaomba msamaha kwa kusema ukweli..
Ona hoja ya 3
Hoja #3
Tendo la ndoa kati ya wanandoa lina malengo makubwa mawili
- Kufurahishana na kujenga umoja kati ya wanandoa
•Kundeleza uzao kwa kupata watoto
Kwahiyo nguvu za kiume mwanaume anatakiwa kuwa nazo kukamilisha hayo malengo
Hoja #4
Tendo la ndoa ni kwa ajili ya mwenzako sio kwa ajili yako.
Wanaume unaposhiriki ni kwa ajili ya kumridhisha mkeo na Mke ni kwa ajili ya kumridhisha mumeo ..
Ukiwa na mtazamo huu utakusaidia kutokuwa mbinafsi na kuwa na tabia ambazo zinamhuzunisha mwenzi wako kwa ajili ya tamaa zako mwenywe
Kila mtu akilenga kumridhisha mwenzake ni mwanzo wa mafanikio kwenye unyumba
Upungufu wa nguvu za kiume ni nini?
Ni pale ambapo mwanaume anashindwa kushiriki tendo la ndoa kiasi cha kumridhisha mkewe..
Soma tena hapo..
Sio kushindwa kufanya kulingana na watu wanavyosema kwamba mwanaume anatakiwa kufanya kwa kiasi gani..
Cha msingi ‘ufanye kiasi cha kutosha kumridhisha mwenzi wako’
Pale unaposhindwa kumridhisha mwenzi wako hiyo inakuwa ni upungufu wa nguvu..
Nasisitiza sio kulingana na kwenye video walivyosema au ulivyoambiwa wengine wanafanya..
Hii itakusaidia sana kuepuka mengi ambayo sio ya mingi yanayotokana na kujilinganisha
Kuna aina mbalimbali za upungufu wa nguvu za kiume
- Kukosa hisia za tendo la ndoa
- Uume kushindwa kusimama imara. Ukisimama unasimama legelege
- Kushindwa kurudia round nyingine kwa muda unaokubalika
- Kuwahi kufika kileleni ‘dakika 1’ imeisha na huwezi kurudia tena
Kuna aina zingine ndogo ndogo kama uume kuwa mdogo sana kiasi cha kutoweza kufanya kazi..
SABABU ZA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME
Kundi la watafiti wa magonjwa ya moyo walihitimisha kwamba ‘Upungufu wa nguvu za kiume’ ni kiashiria kikubwa cha shida kwenye moyo na mishipa ya damu..
Na kwamba mtu asipotibu mapema shida hiyo kwa usahihi ni mtahiniwa wa magonjwa ya moyo na mishipa ya damu.
Hata hivyo kuna sababu mbalimbali za upungufu wa nguvu za kiume. Nazigawanya katika makundi
•Kisaikojia
•Kibaolojia
•Kihomoni (vichocheo)
KISAIKOLOJIA
Je, unafahamu kuwa kiungo kikubwa cha ngono kipo katikati ya masiko yako? Yaani ubongo..
Hapo ndio chanzo cha mambo yote!
Hata kama ukiwa rijali kiasi gani, kichwani ukivurugwa hakuna kitu kitaendelea
Hapa nazungumzia sababu kama
- Stress
Stress ni kawaida kwa mtu mzima, ila zinapokuwa sugu inakuwa ni ugonjwa wa akili ‘sonona’ au depression - Stress za kiuchumi .. muda wote unawaza madeni, unawaza bila kuacha utatokaje kiasi kwamba muda mwingi akili haitulii hata kwenye tendo usishangae huwezi kufanya vizuri..
- Stress za nyumbani, hata kama mwenzi wako anakusumbua hakupi amani hata ile hamasa ya kuwanaye inapotea ni uhakika kuwa hutafanya vizuri
- Kujilinganisha na weengine uliowahi kuwasikia kwamba wanafanya hivi. Au umeambiwa uume unatakikuwa hivi na vile uwe na ukubwa huu au ule.. na wewe ukiangalia hufikii huko inakupa stres unashindwa ku-enjoy
- Kujichua: Huku kuna haribu sana uwezo wa mwanaume kuridhika kwa maana ya kuhamasika kwemye tendo. Inaweza kumfanya mwanaume kuwa mtumwa wa kujichua na kutokuwa na uwezo wa kufanya tendo lenyewe
- Picha za ngono na video: Hizi zinaharibu uwezo wa ubongo kujenga taswira halisi na kupata msisimko wa kutosha kusimamisha kwa muda unaotosha kufanya tendo.
- Uzoefu mbaya: Kuuza mechi ni kawaida mara moja moja.. lakini ukiichukulia kama ndio shida yako au kama mkeo akikutolea maneno mkali inawezakupelekea kutojiamini katika mechi zinazofuata
Naweza kuwa sijasema yote lakini kila kinachofanya akili yako inakuwa haipo kwenye utulivu kuwanacho makini sana kinakuharibia urijali
SABABU ZA KIBIOLOJIA
Uli upate hamu na mashine isimame imara lazima mfumo wa damu, homoni, misuli na neva za fahamu ziwe timamu
Yaani mishipa ya damu iwe na uwezo wa kutanuka kiasi cha kutosha kuruhusu damu kupita ya kutosha ili uume usimame
Na uwe na homoni ya kiume ‘testosterone’ ya kutosha.. hii ni kama mafuta ya kuwasha na kuendesha gari..
Haya mambo mawili yanasaidia misuli laini ya uume isimame imara na kwa muda wa kutosha
Vitu vinavyoharibu mishipa ya damu
- Chakula duni
Ni ajabu mwanaume kula chips..💔 eti kabisa unakula chips jamani sasa nguvu zitatoka wapi..
Huo ni mfano, vyakula ambavyo ni junks.. mafuta mafuta na wanga rahisi kama hizo zinakumaliza..
Matokeo
Yake sio ya leo, pole pole lakini kwa uhakika utaanza kuuza mechi.
- Sigara na pombe
- Vinywaji baridi kama soda na energy drink zinaharibu sana
- Kutofanya mazoezi
- Uzito mkubwa na kitambi
- Kutolala masaa ya kutosha usik
Tabia kama hizo zinaua nguvu za kiume kibailojia kwa sababu zinaharibu mfumo wa homoni na mfumo wa mishipa ya damu na moyo..
Ukiangalia hizo
Sababu zinasababisha pia magonjwa ya moyo na mishipa ya damu ndio hizo hizo zinaleta shida ya nguvu za kiume
DALILI ZA UPUNGUFU WA NGUVU..
Ni kushindwa kumfanya mkeo akuambie asante mume wangu😂
Hakuna uchawi hapo‼️
Mara nyingi hakuna hata haja ya vipimo..
Mimi kwa uzoefu wangu na kushughulika na wanaume kwa miaka sita sasa..
Wapo ambao walifanya vipimo vya bei ghali kuangalia homoni na vitu vingine lakini bila faida.
Ukishaona unauza mechi, kaa chini na mwenzi wako mzugumze.
Wakati mwingine ukute hata shida haipo kwako..
Nimekuambia lengo ni yeye aridhike sio wewe!
Sasa unaweza ukawa umefanya hata nusu saa lakini hajafika.. huoni kuna haja ya kujadiliana kujua shida iko wapi?
Ni kwako au kwake..
Kwa sababu wanawake pia wanamatatizo yao yanayohusiana na unyumba..
Unakuta anamvurugiko wa homoni, uke mkavu, hana hamu kabisa ya tendo yupo tu.. sasa hadi akafika sio mwaka huu
Au unakuta anatabia ya kujichua, nk..
Kwa sababu ni kwa ajili yenu wote kaeni chini mjadiliane shida iko wapi..
MATIBABU YA NGUVU ZA KIUME
Najua hapa ndio unapopasubiri..😋
Kama unashida hiyo zingatia haya..
Moja..
Nguvu za kiume ni shida ya mtindo wa maisha. Hakuna mdudu anayesababisha hiyo shida ni vile tunavyoishi, tunachoingiza kwenye bongo zetu na tunachoingiza kwenye midomo yetu.
Mbili..
Usiwe na haraka ya kutafuta dawa..
Ni kweli unapokuwa kwenye shida unakuwa unatakani kupata majibu chap chap hiyo itakuponza..
‘Kaa chini na mwenzi wako tafuta sababu’
Kama bado mashirikishe daktari anayefahamu hayo masuala akusaidie kujua shida ni nini sio akupe dawa..
Hii ni kwa sababu unaweza kukuta shida yako ipo kwenye akili sasa utakuwa dawa gani kutibu mitazamo na stress?
Tatu..
‼️‼️ Usitubutu kunywa Viagra (sildenafil)
Kijana umenisikia..
Zinaweza kukuletea shida kubwa ya moyo kama ilikuwa imeanza tayari bila wewe kujua
Na inakufanya unakuwategemezi wa dawa. Itafika mahali bila viagra kaka hata hastuki..
Na itafika mahali hiyo dawa yenyewe haifanyi kazi.. hapo ndio utaomba Yesu arudi.
Nne..
Nguvu za kiume zinatibika kwa asilimia 100% hii ndio habari njema!
Fanya haya mambo nitakayokueleza hapa chini!
MAMBO MUHIMU KURUDISHA NGUVU ZA KIUME MILELE
- Jifunze kutawala msongo
Msongo ni sehemu ya maisha ya mwanaume, jifunze kutawala misongo inayokuhusu..
Tafuta majibu kwa changamoto zinazokukabili
- kula chakula hai
Chakula hai ni chakula ambacho kwa sehemu kubwa kimetokana na mimea katika uasili wake
Achana na kula vyakula kama:
- Nafaka zilizokobolewa
- Vyakula vyenye sukari rahisi
- Vinywaji kama soda, pombe, energy drink
- mikaango kama chips
- Junks kama chapati za ngano zilizokoblewa, chapati, vitumbua nk
Pendelea sana sana kula
- Matunda kwa wingi na mbogamboga kama zote
Hapa nikuibie siri
Matunda na mbogamboga hasa mbichi kama kachumbari zina nitric oxide ambayo ni viagra ya asili.
Ukivutumia kwa wingi ndani ya wiki utaanza kuona kuna namna heshima inarudi
Jinsi rahisi ya kufanya..
Asubuhi kula matunda mengi ya kutosha.. halaf nenda ukapige kazi zako..
Mchana na jioni: Anza kula kachumbari ya kutosha kisha kula chakula kingine
Usiku kama unaonaona huna njaa sana kula bakuli kubwa la kachumbari (salad) ya mbogamboga kama nyanya, karoti, pilipili hoho, vitunguu maji nk
Mbinu ya nyongeza kwenye chakula:
‘Tengeneza chai ya mbegu za maboga’
Kaanga mbegu za maboga halaf zisage kwenye brenda au utakavyoona inawezekana..
Tumia kijiko 1 cha huo unga kwenye chai au maji ya moto kikombe1..
Kunywa asubuhi na jioni.. siku 2 utasikia mlingoti chuma
Ukifanya na chakula hai kama nilivyokuambia huna haja ya kulipa laki 3 kununua mitishamba.
Mambo mengine ya kufanya
- Pata angalau dakika 30 hadi lisaa la kufanya mazoezi.
- Acha uvutaji wa sigara na kunywa pombe
- Acha kuangalia picha na video za ngono
NB: Kuna product ambazo zinasaidia kuimarisha urijali.. zipo janja janja na nzuri ..
Kuwa makini unapochagua products kama hizo na unapotumia sio mbadala wa hayo niliyokuambia na mara nyingi hakuna haja kabisa ya hizo dawa..
Nikukimbie sasa
Nisamehe kwa kukundikia kitabu badala ya somo😂😂
Mungu akujalie, ukafanikiwe shemeji afurahie tena kukuchagua💪
Dr Nature
Nahitaji mawasiliano yako Dr. Nature
+255767759137