Faida Ya Mbegu Ya Parachichi – Jinsi ya Kuandaa na kutumia

FAIDA ZA MBEGU ZA PARACHICHI, MAGONJWA YANAYOTIBIWA NA UNGA WA MBEGU ZA PARACHICHI

Limetumika kwa miaka mingi kama tunda na pia kama mboga. Kwa sababu ya wingi wa virutubisho vyake linatumika kutibu maradhi ya shida ya mmeng’enyo wa chakula, moyo na mfumo wa damu, urutubishaji wa nywele na ngozi, na kuboresha afya.

Mbegu yake inatumika katika tiba, zamani walikuwa wanatumia kutengenezea wino wa kuandikia. Lakini leo imegundulika kuwa na faida lukuki.

FAIDA YA MBEGU ZA PARACHICHI

Virutubisho kwenye kijiko 1

Vitamin K 26% ,Folate 20%, Vitamin C 17%, Potasimu 14%, Vitamin B5 14%, Vitamin B6 13%, Vitamin E 10%. Virutubisho vingine ni Magnesium, manganese, shaba, chuma, zinki, phosphorus, vitamin A, B1, B2 na B3. (asilimia ni kiwango cha kirutubisho kinachotakiwa kwa siku).

70% ya faida zote za parachichi zipo kweye mbegu yake.

Kwahiyo unapokula parachichi na kutupa mbegu yake unakuwa umekula faida 30% na kutupa 70%, hasara iliyoje.

Faida:

  1. Inapambana na mioto katika mwili na kutibu magonjwa yanayohusiana na mioto kama shida kwenye jointi za mifupa, arthritis.
  2. Inasaidia mfumo wa mmeng’enyo wa chakula na hivyo kutibu shida ya gesi tumboni, kuendesha, kuvimbewa na madonda ya tumbo.
  3. Husaidia uzalishwaji wa kolajeni na hivyo kukusaidia usizeeke mapema na ngozi yako kuonekana vizuri bila mikunjo. Hufanya kazi ya kulainisha na kung’arisha ngozi pia.
  4. Inaimarisha kinga ya mwili na kukuweka mbali na magonjwa. Itakusaidia kutopoteza muda kushughulika na magonjwa yako au kutenga pesa ya kumwona daktari kwa ajili ya magonjwa madogomadogo.
  5. Hutibu presha ya chini na ya kupanda. Dalili za presha ya chini ni pamoja na kizunguzungu, maumivu ya kichwa, kupoteza faham, moyo kwenda kasi. Inasababishwa na kuwa na msukumo mdogo wa damu kwenye mishipa ambao inawezakuwa inachangiwa na kuwa na magonjwa sugu, magonjwa ya figo, upungufu wa damu, kisukari na utapia mlo.
  6. Husaidia katika maradhi ya moyo.

Mgonjwa wa moyo anatakiwa kula maparachichi ikiwa ni pamoja ana mbegu yake. Unga wa mbegu yake anaweza kuwekakwenye chai, juisi, smoothie hata maziwa.

  1. Hutukinga dhidi ya saratani. Mbegu za parachichi zinasaidia seli za saratani kujiua.

Yaani virutubisho vya mbegu ya parachichi ni maadui wakubwa wa saratani. Seli zikiona tu hivyo virutubisho vimekuja, basi zinaamua kujiua.

  1. Hutibu maumivu ya mifupa na misuli
  2. Inasaidia kuunguza mafuta na kukusaidia kupunguza uzito haraka
  3. Huondoa sumu mwilini

Maandalizi:

Ondoa ganda la nje la mbegu, kisha kwangua kupata unga.

Anika sehemu isiyo na mwanga wa jua la moja kwa moja. Inaweza kuchukua hadi siku 6 kukauka kabisa. Ili kupata unga mzuri unaweza ukatwanga baada ya kuwa imekauka au ukatumia mashine.

Tunza kwenye chupa isiyoruhusu mwanga. Unaweza ukatunza kwa muda mrefu bila kuharibika.

Matumizi:

Kwa ajili ya chai:

Weka kijiko 1 chai chai na kijiko 1 cha asali kwenye kikombe. Kunywa kutwa mara 3. Hapo faida zote unakuwa umezipata.

Unga wa mbegu za parachichi sio wa kuchemshia na maji, weka kwenye chai au kinywaji ambacho kinakuwa tayari kwenye kikombe.

Kama hutumii kama dawa, unataka kutumia kama chakula kawaida kila siku, ongeza kwenye maziwa, chai, juisi, smoothie au mboga kadri unavyotaka.

Kwa ajili ya chai au vinywaji vingine unaweza ukanogesha kwa radha za viungo vingine kama iliki na mdalasini

Kwa ajili ya urembo:

Shared with ❤️

Dr. Nature

••••••••••••••••••••

Kwa Tips zaidi jiunge na channel ya WhatsApp: https://whatsapp.com/channel/0029VaDNpvoA2pLHZYrJOK2B

0 0 votes
Article Rating
Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Share
Scroll to Top