Vyanzo Vya Maji Ya Kunywa Na Usalama Wake

VYANZO VYA MAJI YA KUNYWA NA USALAMA WAKE

Na Umuhimu Wake Katika Kupunguza Uzito

Imezoeleka kusikia ushauri kuwa kunywa maji mengi yanasaidia kupunguza uzito.

‘Ni Kweli’..

Kivipi?

 • Kadri unavyokunywa maji zaidi unapunguza kiasi cha vinywaji baridi kama soda utakavyo kunywa.

Ukinywa maji mengi unapunguza kiasi cha soda au energy drink ambacho utakunywa. inatokea ‘automatically’.. hii inakusaidia kukupunguzia mafuta yanayotunzwa

 • Maji yanapunguza kiwango cha homoni ya ‘angiotensin’.

Hii ni homoni ambayo inahusika na kuongeza KIU ya maji na kupandisha presha ya damu pale ambapo figo zinapogundua upungufu wa damu inayofika maeneo ya pembeni ya mwili.

Hiyo homoni inafanya mishipa ya damu isinyae ‘contract’ na hivyo kuongeza presha ili damu ifike sehemu za mbali zaidi.

Matokeo mengine ya angiotensin ni kuwa inasababisha KUTUNZA MAFUTA zaidi.

Ukinywa maji ya kutosha unaongeza kiasi cha damu na hii homoni inazalishwa kwa uchache na hivyo mafuta hayatunzwi zaidi

 • Matumizi ya maji zaidi inaonekana kusaidia watu kula vizuri zaidi. Watu wanaokunywa maji ya kutosha kila siku wanakula zaidi matunda mbogamboga na nafaka zaidi ambavyo vinapunguza uzito kwa ufanisi.
 • Maji yanatumika katika mchakato wa kuchoma mafuta. Kama umewahi kutumia ‘Easy chopper’ dawa ya kupunguza uzito utakuwa shahidi, wa jinsi kiu unavyoongezeka.

Shughuli za mwili ‘metabolism’ zinahitaji maji mengi ili zifanyike kwa ufanisi ikiwemo kuchoma mafuta.

Kwa kuwa kupunguza uzito milele lazima uzingatie usalama na afya kwa ujumla muhimu ufahamu vyanzo bora vya maji.

VYANZO VYA MAJI KWA UBORA

 1. Chakula hai

Asilimia 70 hadi 95 ya matunda na mbogamboga ni maji. Unapokula kwa wingi umekula maji.

 1. Maji ya chemchemi

Ni maji mazuri yenye madini ya ardhini. Kutokana na uchafuzi unaoendelea ni vema maji chanzo kiwe kimepimwa kuwa ni salama na maji yachemshwe.

 1. Maji ya mvua

Kutegemeana na namna ulivyoyavuna, inaweza ikahitajika kuyachuja kwa vifaa maalumu filters au pitchers.

Na wakati mwingine ni vema ukayachemsha kabla ya kuyanywa.

 1. Maji ya bomba

Ni maji safi lakini yana kemikali nyingi zinazotokana na mchakato wa kuyatibu. Ni vema ukayachuja kwa filters au pitchers.

 1. Maji ya chupa

Ni ya mwisho kwa usalama! Kutokana na kemikali zinazoingia kwenye maji kama microplastics nk.

Yatumia tu pale ambapo ni lazima sanaaa!

UNYWE KIASI GANI?

Ikiwa hauna shida ya moyo wala ugonjwa wa figo.. fanya hivi:

(Hiki ni kiasi ambacho unatakiwa kunywa kwa siku)

NB: Sio wazo zuri kunywa maji mengi sana kwa mara moja. Weka kwenye chombo chako unywe kidogo kidogo

Wanawake:

 • Miaka 9-13: Vikombe 7
 • Miaka 14-18: Vikombe 8
 • Miaka 19+: Vikombe 9

Wanaume:

 • Miaka 9-13: vikombe 8
 • Miaka 14-18: vikombe 11
 • Miaka 19+: Vikombe 13

Nimeona wengi hata mama yangu wakipona magonjwa yaliyowasumbua muda mrefu kwa kunywa maji.

Kunywa maji!

Kunywa maji!

Jitahidi usishau kunywa maji!

Mungu akubariki..

Shared with ❤️
Dr Nature

•••••••••••••••••••••••
Kwa tips zaidi ni follow kwenye whatsapp channel: https://whatsapp.com/channel/0029VaDNpvoA2pLHZYrJOK2B

0 0 votes
Article Rating
Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Share
Scroll to Top