Kwanini ni muhimu kujifunza hili?
Kuna sababu mbili kubwa kwanini mwanamke ajli uzito wake kabla ya kupata ujauzito; afya ya mama na afya ya mtoto.
Hasa kwa jamii yetu ambayo mimba sio kitu cha kupanga inakuwa kama surprise ya mwanamke kutoona siku zake. Ni muhimu sana kufahamu jambo hili muhimu.
Uzito mkubwa na kitambi kabla ya kubeba mimba ina madhara makubwa sana kwenye afya ya mama na afya ya moto akiwa tumboni na hata baada ya kuzaliwa.
Kufahamu hili itakusaidia kuwa kujikinga na madhara yanayotokana na uzito mkubwa wakati wa ujauzito kwako na kwa mtoto.
Kuna magonjwa mabayo mama anaweza kuyapata wakati wa ujauzito kwa sababu tu ya uzito mkubwa na kitambi.
Na pia kuna magonjwa ambayo mtoto anaweza kuzaliwa nayo pale anapozaliwa na mama mwenye uzito mkubwa na kitambi. Kama haitoshi, inawezekana mama akamtengenezea mazingira ya mtoto kuwa na uzito mkubwa na kitambi katika maisha yake yote kwa sababu ya vile alivyokuwa wakati wa ujauzito.
Katika sehemu ya uzito mkubwa kabla ya ujauzito, nitajikita kukuonesha umuhimu na namna ya kupunguza uzito kabla ya kubeba mimba.
Kufuatia elimu hii, ni muhimu kila wenzi mnapotaka kupata mtoto mpate muda wa kuajiandaa kutengeneza mzingira mazuri kwa ajili ya mtoto atakayepatikana awe na afya njema. Na hiyo itamtenenezea msingi wa kuwa na afya njema katika maisha yake yote kwa ujumla.
Kwanini upunguze uzito kabla ya kubeba mimba?
Hadi unakuwa na uzito mkubwa na kitambi, tayari mfumo wako wa homoni hauko sawa. Kuna homoni ambazo zipo juu kama estrogen na insulin aambazo zinaathiri pia homoni zingine.
Homoni ni vichocheo vya mwili ambavyo vinasaidia kazi za mwili ziweze kufanyika inavyotakiwa. Zikiwa hazipo kwenye uwiano mzuri yaani kuna homoni zimezidi an nyingine zimepungua utapata ugonjwa au shida ya kiafya kulingana na hiyo homoni inafanya kazi gani.
Ukiwa na uzito mkubwa na kitambi, homoni nyingi huwa zinavurugika. Miongoni mwa homoni hizo ni homoni za uzazi kwa wanaume na wanawake.
Kwa wanaume, estrogen ikiongezeka (estrogen ni homoni ambayo ipo kwa wingi sana kwa wanawake kuliko kwa wanaume) inaleta madhara kwenye nguvu za kiume. Ndio maana utaona wengi wenye uzito mkubwa au kitambi wanapata changamoto sana kitandani.
Kwa wanawake, Mfumo wa homoni ukivurugika madhara yanayoweza kutokea ni pamoja na;
- Mpangilio wa hedhi kuvurugika.
Unapata hedhi ambazo hazina mapingilio. Kuna miezi mingine unavuka kujaona siku zako, kuna miezi mingine unaingia mara mbili. Kuna wakati unaona damu nyingi sana tena kwa siku zaidi ya 7. Na hedhi inakuwa kama ugonjwa kwa sababu inakuwa na maumivu makali.
- Uvimbe kwenye kizazi na mifuko ya mayai ‘ovaries’. Uvimbe unaweza kuwa fibroids au viumbe maji ‘PCOS’.
- Ukavu ukeni.
Tendo la ndoa linakuwa halina radha tena hata kama ujiandae au uandaliwe kiasi gani
- Kukosa hamu ya tendo la ndoa.
Kwenye mahusianoya ndoa unakuwaunafanya tu kumridhisha mwenzako ila upo tu huna hamasa yoyote. Muda wote siku zote za mwezi huna hamu na hata kileleni huwezi kufika.
- Kushindwa kushika mimba.
Unapokuwa na shida ya kutaka kupata mtoto; unaweza ukafanya vipimo vyote ukaambiwa uko sawa. Ila kama una uzito mkubwa, ukipunguza tu uzito chap unashika mimba. Hii ni kwa sababu uzito mkubwa unavuruga mfumo wako wa homoni.
- Mimba kuharibika.
Ukishika mimba ukiwa na uzito mkubwa na kitambi kuna uwezekano wa mimba kuharibika, ikaporomoka kabla ya wakati.
Kuna vyanzo vingine vingi vya mimba kuharibika; uzito mkubwa ni kihatarishi mojawapo.
Namna ya kupunguza uzito kabla ya kubeba mimba
Iwe ni ndoa changa au tayari mna mtoto mnataka kuongeza mwingine, jengeni tabia ya kupanga lini mnataka kuwa na mtoto. Inawezekana kwa sababu kuna njia aina nyingi sana za uzazi wa mpango ambazo mnaweza mkazitumia kuzuia kutopata mtoto kwa kipidi ambacho mnajijenga.
Hii itawasaidia mpate muda wa kutosha kuandaa mazingira ya kiafya, kiuchumi na kijamii kwa ajili ya kuleta mimba na mtoto atakayezaliwa. Epukeni mambo ya kushutuka tu ..’’oh mume wangu mwezi huu sijaona siku zangu, nina mimba nini..?’’ hahahaahah.
Fahamu lengo la uzito wako. Yaani kulingana na urefu wako unatakiwa kuwa na uzito kiasi gani. Kama uzito wako upo sawa, basi ni jambo jema. Kazi yako ni kuulinda usiongezeke kupita kiasi kinachotakiwa wala kisipongue sana pia ikavuka mstari wa chini.
Ikiwa umegundua una uzito mkubwa, kuna mambo machache unaweza ukafanya yakakusaidia kufikia lengo la uzito wako kabla ya kubeba ujauzito. Mambo haya yamewasaidia mamia ya wanawake niliowafundisha. Sio tu kwamba ni njia rahisi lakini pia ni njia ambazo zinafanya kazi kwenye kila aina ya mwili wa mwanamke.
Urahisi wake ni kuwa kila mmoja anaweza akafanya lakini ugumu wake ni kuwa inakuhitaji nidhamu, uvumilivu na kujitoa ili kufanikisha kufikia lengo lako. Sikuahidi kwamba ukitumia njia hizi itakuwa rahisi sana, lakini ambacho nakuahidi ukifanya mambo haya utapungua kiafya na kufikia lengo lako.
- Chagua kwa umakini njia za uzazi wa mpango
Njia za uzazi wa mpango ni njia ambazo kama wenzi mnaweza kuzitumia ili kuzuia msipate mtoto katika wakati ambao hajawa tayari. Kama mnaishi pamoja ni wazi kwamba lazima mtasalimiana mara kwa mara. Kama hakuna njia ambayo itawasaidia kupanga uzazi mnaweza kujikuta mna pata watoto katika wakati ambao mlitaka kusubiri.
Kuna njia aina nyingi lakini nazigawa katika makundi mawili; njia zinazotumia homoni na njia zisizotumia homoni.
Njia zinazotumia homoni ni njia za uzazi wa mpango ambazo zinakuwa na homoni ambazo zinaingizwa kwenye mwili wa mwanamke. Homoni hizo zinafanya kazi ya kubadilisha mfumo wa homoni wa mwanamke kuwa katika namna ambayo mwanamke hawezi kubeba ujauzito.
Matokeo ya hizo njia inakuwa ni kuvuruga mfumo wa homoni wa kawaida lakini katika namna ya kitaalamu. Ndio maana utaona side effects kwa baadhi ya wanawake ni kuongezeka uzito, hedhi kuvurugika, kutoona siku kabisa, kutokwa damu nyingi na shida ya kupata mtoto pale unapohitaji kubeba mimba.
Mfano wa njia hizi ni vidonge, sindano na vipandikizi.
Kwa kawaida kuchagua njia ya uzazi wa mpango ni lazima umshirikishe mwenzi wako pamoja na mtaalamu wa afya. Mimi ningekushauri usitumie kundi hili la njia za uzazi wa mpango kama unaweza kutumia njia za uzazi w ampango ambazo hazina homoni.
Kundi lingine ya njia za uzazi wa mpango ni zile ambazo hazitumii homoni. Katika kundi hili kuna njia za kudumu kama upasuaji w akufunga mirija ya uzazi na njia za muda mfupi.
Kwa kuwa unataka kuchagua njia ya uzazi wa mpango ili baadaye upate mtoto utachagua njia ambazo sio za kudumu. Njia hizi ni pamoja na kutumia kalenda, kumwagia nje na kitanzi.
Kabla ya kuchagua njia yoyote ya uzazi wa mpango, jadiliana na mwezi wako pamoja na mtaalaam wa afya kupima faida na hasara za njia hiyo ili kuona njia ambayo itafaa zaidi kwenu.
Ikiwa ni lazima kuchagua njia inayotumia homoni; baada ya kuwa umemaliza matumizi yake, nashauri tenga angalau miezi 3 ya kurekebisha mfumo wa homoni kabla ya kubeba ujauzito.
- Chakula hai
Chakula hai ni mfumo wa chakula ambacho kwa sehemu kubwa kinatokana na mimea katika uasili wake. Kuna mana tofuati ya kupangilia kulingana na mahitaji na lengo binafsi lakini kwa ujumla, mfumo huu unahusisha kula wingi wa vyakula vinavyotokana na mimea katika uasili wake.
Hii hapa ni namna rahisi sana ambayo unaweza ukaanza nayo;
Asubuhi:
Usile kitu kingine chochote isipokuwa matunda. Kula matunda mengi hadi ushibe. Kula matunda aina yoyote yanayopatikana unayoweza kununua.
Mchana na jioni:
Tengeneza saladi ‘kachumbari’ . Hii ni mchanganyiko wa mbogamboga ambazo unaweza ukala zikiwa mbichi. Mfano wa mbogamboga hizi ni nyanya, karoti, pilipili hoho, tango, parachichi, nazi, beetroots, kabeji, vitunguu maji nk.
Kula kachumbari ya kutosha kabla ya kula chakula kingine abacho huwa unakula. Chakula hicho kinafaa sana kama kikiwa kimetokana na mimea
Sehemu hii ya chakula inabeba asilimia kuwa ya kukusaidia ufikie lengo lako
- Mazoezi
Fanya mazoezi unayoyapenda asubuhi kabla hujala chochote angalau mara moja kwa siku kwa siku nyingi zisizopungua 5 kwa wiki.
Mazoezi unayoweza kufanya ni pamoja a kutembea, kukimbia, kuendesha baiskeli, kucheza, kunyanya uzani, kuruka kamba, kucheza mpira nk.
- Usingizi
Kulala usiku masaa 7-8 inasaidia kuongeza kasi ya mwili kuchoma mafuta mara 2. Jitahidi kupata muda wa kutosha kila siku kulala masaa ya kutosha usiku.
- Easy chopper
Hii ni bidhaa ya fomula ya asili ambayo inasaidia kuongeza kasi ya mwili kuchoma mafuta. Sio chungu wala sio ya kuharisha. Inasaidia kupunguza njaa na kuchoma mafuta na hivyo inasaidia kupunguza uzito na kitambi kirahisi.
Inawezekana suala la chakula hai na mazoezi vinakupa changamoto. Easy chopper inaweza kukusaidia kufikia lengo lako.
Kama tayari unafanya chakula hai, mazoezi na unalala vizuri ukitumia easy chopper inakuboost ili uweze kufikia lengo lako kwa haraka zaidi.bh