Kula Kulingana na Kundi la Damu – Kuna Faida Yoyote?

TULE KULINGANA NA MAKUNDI YA DAMU?

Hii nadharia alianzisha na baadhi ya wataalamu wa tiba asili na kuungwa mkono na wataalamu wengine baadaye.

Unafahamu mara nyingi wataalamu wa tiba asili hawategemei sana sayansi, wanategemea kile ambacho kina leta majibu na vile mtaalamu atakavyowaza inafaa au kilichozoeleka kuwa kinasaidia.

Lakini katika ulimwengu wa sasa tunataka ushahidi wa kisayansi kama ni kweli..

Hakuna ushahidi wowote wa kisayansi unaoonesha kwamba watu wale chakula kulingana na makundi ya damu..

Kwamba eti ukiwa group O usile moja mbili tatu..

Kinachoonekana ni kuwa kila mtu bila kujali group lake la damu anatakiwa kula chakula hai. kinamsaidia kukinga na kutibu magonjwa yote.

Naunga mkono kwa ufahamu wangu hili kwa sababu..

Moja..

Ninaamini nimeumbwa na Mungu.. na hivyo chakula ambacho Mungu aliwapatia watu wa mwanzo ni kile kile kwa kila mtu.. sitaki kuamini Adam, Hawa na watoto wao walikuwa na group moja wa damu😂

Au Mungu angesema adamu utakula matunda X lakini mkewe atakuwa Matunda Z Ila watoto wkao wasile matunda wale mizizi tu kwa sababu wao ni group tofauti😂

Achana na hao.. Njoo hapo kwako

Wewe na mwenzi wako na watoto si ajabu mna magroup tofauti ya damu..

So mkipika chakula kuwe na aina ya vyakula aina nne tano, ili kila mtu ale cha kwake🤔

Mmh ..

Haiko hivyo, kula chakula hai achana na mambo ya kula kulingana na magroup ya damu hayana uthibitisho wowote!

Ni kama umewahi kusikia baadhi ya wataalamu wa tiba asili wanafundisha kwamba ukitaka kupona kiungo chochote tafuta mmea unaofanana na hicho kiungo ndio dawa😂

Mfano, kama mwanaume unashida ya maumbile kula tango😂

Una upungufu wa damu kula nyanya, beetroot, rosella nk😂

Inaweza ikawa inasaidia kwa sehemu lakini usiitegemee kwa upofu, fahamu sayansi halisi inasemaje..

Dr Nature

0 0 votes
Article Rating
Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Share
Scroll to Top