Tiba Ya UTI Sugu Kwa Siku 3 Kwa Vitu Viwili (Nyumbani)

UTI ni kirefu cha maneno ya kiingereza (Urinary Tract Infection) yenye maana ‘Maambukizi Kwenye mfumo wa mkojo’.  Maambukizi haya yanaweza kuwa ya bakteria (mara nyingi zaidi), fangasi na virusi.

Mara nyingi mfumo wa mkojo una bakteria walinzi na kila siku unapanda lundo la bakteria wageni kutoka nje. Lakini kinga ya mwili inapambana na wageni na kuwashinda. Pale uwezo wa kinga yako unapokuwa dhaifu kupambana, basi wageni hawa wanasababisha madhara.

Mfumo wa mkojo unajumuisha figo, mirija inayotoa mkojo kwenye figo inaitwa ureters, kibofu cha mkojo na mrija unatoa mkojo kutoka kwenye kibofu kwenda nje unaitwa urethra. Ukipata maambukizi popote katika sehemu hizi unakuwa umeugua UTI.

Wanawake waathrikika zaidi ya ugonjwa huu kwa sababu ya namna maumbile yao yalivyo. Njia ya mkojo kutoka nje kwenda kwenye kibofu cha mkojo ni fupi sana tofauti na wanaume.

Vile vile, kwa maumbile yao ili kupata haja inawalazimu kuchuchumaa na hivyo kuwa rahisi kupata haya maambukizi kirahisi.

Dalili za UTI

Sio lazima upate dalili zote, lakini hizi ni dalili unazoweza kupata ukiwa na UTI.

  1. Kukojoa mara kwa mara licha ya kuwa hujanywa maji mengi
  2. Maumivu wakati wa kukojoa
  3. mkojo kuwa na harufu mbaya na unaweza kubadilika rangi na kuwa na rangi ya kahawia hadi nyekundu
  4. Maumivu ya tumbo
  5. Unaweza kupata homa wakati mwingine maumivu ya kichwa

Tendo la Ndoa Linaweza Kueneza UTI?

Ndio. 

Tendo la ndoa hasa pale via vya uzazi vinapokutana, kuna uwezekano w akuhamisha bakteria au vimelea wanaosababisha ugonjwa huu kwenda kwa mwenzi. Hata hivyo kwamba mwezi atapa ugonjwa au la inategemeana na kinga ya mwili wake na dozi ya bakteria aliowapata kwa mgonjwa.

Inabaki kuwa ushauri mzuri zaidi kutibu kikamilifu ili kuepusha kumwambukiza mwenzi wako.

Nini Kinasababisha UTI Kuwa Sugu (Kujirudia rudia)

  1. Kutomaliza Dozi

Inawezekana umewahi kutibiwa, baadaye ukajisikia vizuri dawa hukumaliza. Hiyo ni tabia mbaya, inawafanya bakteria wanakuwa sugu. Na matokeo yake ukijakuugua tena ukatumia hizi dawa bakteria wanazishangilia hazikusaidii.

Ukiandikiwa dawa hakikisha unamaliza dozi kwa uaminifu hata baada ya kujisikia vizuri. 

2. Kutotumia dawa sahihi

Imekuwa kawaida ya wengi wetu kwenda tu kununua dawa pale unapojisikia dalili ya ugonjwa. Magonjwa yanafanana sana dalili unaweza ukadhani unaugonjwa fulani lakini bila kupima uwezekano ni mkubwa wa kukosea na ukatumia dawa ambayo sio ya ugonjwa huo.

Matokeo yake ni kujenga usugu wa dawa kwa hawa wadudu na utakuwa hauponi UTI kila wakati. 

Kwa kawaida inatakiwa uende kupima na hasa bakteria waoteshwe ili kujua ni bakteria gani na anasikia dawa gani ndio upewe dawa. Lakini kwa sababu ya umasikini, serikali imetoa mwongozo wa dawa za kutumia kulingana na aina ya bakteria inayoathiri wengi wetu.

Ni vema kupata matibabu kwa daktarikwa sababu kila wakati tafiti zinafanyika na dawa elekez zinabadilishwa. Usiende tu kununua dawa kwa sababu jirani au ndugu yako ilimsaidia. Nenda kapime upewe dawa sahihi.

3. Kinga Duni

Kutokana na mtindo ovyo wa kinga ya mwili UTI inakuwa ya kujirua rudia. Kwa sababu kila siku tunakutana na bakteria hatuwezi kukwepa ni lazima kinga zetu ziwe imara.Ukiwa na kinga kidogo huna ulinzi hata bakteria kidogo tu kwako ni shida.

Mambo yanayoshusha kinga ya mwili ni;

  • Lishe Duni: Kula sukari, mafuta mabaya, kutokula matunda na mbogamboga za kutosha. Ili kuimarisha kula chakula hai.
  • Madawa: Dawa za uzazi wa mpango, antibiotics au kama unatumia dawa za muda mrefu za ugonjwa wowote zinashusha kinga ya mwili. Tiba kwa njia za asili zaidi ili kupunguza au kuepuka madawa.
  • Kutofanya mazoezi
  • Magonjwa: Ukiwa unaumwa magonjwa hasa sugu kama kisukari, presha, moyo na figo yanashusha kinga ya mwili.

Dawa ya UTI Sugu, Tiba Nyumbani Kwa Siku 3

UTI ni maambukizi kwenye njia ya mkojo.  Mara nyingi yanasababishwa na bakteria japo vimelea wengine pia wanaweza kusababisha. 

Mahitaji:

🧅 Vitunguu maji 4 vikubwa 

📍 Baking soda (bicarbonate of soda)

💧 Maji lita 1 na nusu

Maelekezo

Katakata Vitunguu kisha vichemshe kwenye maji hayo lita 1.5 kwa dakika 10. Kisha acha ipoe ukiwa umefunika.

Chuja na tunza kwenye chombo safi chenye mfuniko. 

Matumizi:

Chukua kikombe 1 cha maji ya vitunguu ongeza nusu (1/2) kijiko cha chai cha baking soda. Koroga vizuri nakunywa. 

Fanya hivyo asubuhi na jioni kwa siku 3-5.  Kwa uwezo wa Mungu utakuwa umepona. 

Tahadhari

Wajawazito na watoto chini ya miaka 6 wasitumia dawa hii. Kwa watoto zaidi ya miaka 6 pata usaidizi wa daktari wetu.

Jinsi ya Kujikinga na UTI

✅ Hakikisha unakunywa maji ya kutosha yasipungue lita 2 kwa siku. 

✅ Dumisha usafi

✅ Kula chakula hai itakusaidia kutengeneza kinga nzuri

🚫 Epuka pombe na sigara

❗️ Nenda kakojoe baada ya tendo la ndoa (mwanamke)

❌ Acha matumizi ya dawa za uzazi wa mpango hasa zinazotumia homoni. Tumia njia za asili. 

0 0 votes
Article Rating
Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Share
Scroll to Top