Kwanini KUJINYIMA Chakula Sio Njia Nzuri ya Kupunguza Uzito na Kitambi Milele?
Watu wengi huenda na wewe ni miongoni mwao wanaamini kuwa wamenenepa kwa sababu wamekula sana.
Na hivyo ili wapungue walazimishe kupunguza kula (kiasi cha chakula)-
‘Washinde na njaa’
Siku zote, kitu kinachoweza kukupatia matokeo ya kudumu ya kupunguza uzito mkubwa lazima kiwe na sifa tatu;
⏩️ Kiwe kinaleta matokeo ya kuchoma mafuta
⏩️ Kiwe salama kiafya
⏩️ Kiwe endelevu, yaani unawez an ukakifanya kila siku katika maisha yako
Ukitazama KUJINYIMA ina sifa moja tu, kuchoma mafuta! Zingine zote inakosa.
Kuna aina ya kujinyima inaitwa kufunga kwa muda mfupi ‘intermittent fasting’ ambayo ni nzuri sana kiaya lakini kujinyima huko ambako vibonge wengi wanafanya sio salama kiafya.
Mtu anashindia juisi (anaogopa kula) licha ya kuwa njaa inamuuma.
Wengine hawapungui kabisa kwa sababu ameshinda na njaa siku nzima mlo wa jioni anavyokula anafidia vya siku nzika na zaidi🤔
Wanaopungua WANAKONDA sio kupungua kupendeza.
- Ngozi inapauka na kujikunja
- wanakuwa hawana nguvu wanajisikia uchovu uchovu
- wanapata vidonda vya tumbo
- na kero kero nyingi
Kwa sababu hali vizuri wanakosa virutubisho
Kama kitu sio salama kiafya na unapambana na asili, hakiwezi kuwa endelevu.
Umeona wengi huenda hata na wewe uliacha ukakata tamaa ukasema liwalo na liwe.
USIOGOPE!
Unaweza ukapunguza uzito na kitambi huku unakula kadri unavyotaka✅
Hivi ndio ninavyofundisha na mamia ya watu wameshuhudia. Unachotakiwa ni kula CHAKULA HAI.
Kama hufahamu chakula hai ni kipi maelekezo haya hapa BURE!!
Shared with ❤️
Dr Nature