Parachichi ‘Ovacado’ Inanenepesha?

Parachichi kama ilivyo vyakula hai vingine vinaufanya mwili uwe na afya njema kwa ujumla.

Matumizi ya chakula hai yanakusaidia kuwa na mwili wako katika ubora zaidi.

Ikiwa umedhoofu umekuwa na uzito mdogo sana inakusaidia kukuongezea uzito ufikie uzito unaokustahili.

Nimeona kwa wagonjwa kama wagonjwa kisukari waliokuwa wamekonda kwa sababu ya ugonjwa wametumia parachichi miongoni mwa vyakula hai vingine na wameongeza uzito.

Wanaofanya program za kuongeza uzito wanashauriwa pia kutumia parachichi mojawapo ya tunda linalosaidia kuongeza uzito huku ukutunza afya yako.

Kwa upande mwingine parachichi linakusaidia kupunguza uzito.

Ikiwa una uzito mkubwa kwa sababu ya mafuta mengi ya ziada au una kitambi.. parachichi ni mojawapo ya matunda mazuri unayoweza kuyatumia.

Unaweza ukatumia parachichi kama tunda au ukachanganya na kachumbari ukawa umelitumia kama mbogamboga.

Hujafurahia faida zote za parachichi kama hujatumia mbegu yake, nimeshafundisha hapa.

0 0 votes
Article Rating
Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Share
Scroll to Top