Kwenye yai moja lililochemshwa unapata
- kalori: 80
- Mafuta Kwa ujumla: 5 g ambapo ‘Saturated fat’ ni 1.6 grams
- Kolestro: 200 mg
- Wanga: 0.6 gram
- Protein: 6 grams
- Nyuzi lishe: 0
- Vitamin na madini
Nimeanza na kukuonesha vitu unavyovipata kwenye mayai ili nitakachokueleza kiwe na maana kwako.
Tuchukulie mfano, wewe unakula mlo wa asubuhi unaojumuisha Mayai na kachumbari. Ni namna ambayo wengi hufanya.
Mlo huu hauna wanga wala sukari kwa sababu kwenye mayai hakuna wanga (uliopo hauna mashiko) na kwenye kachumbari wanga wake ni kidogo sana kiasi kisicho na mashiko.
Kama hakuna sukari kwenye mlo wako, amani inakuwepo kwamba haitakuletea shida kwenye uzito au kitambi.
Hii ni kweli kama haya mambo niliyokueleza hapa chini hayatatokea!
Anzia hapa…
Hadi unaongezeka uzito au ukawa na kitambi tayari una usugu wa insulin ‘insulin resistance’.
Insulin ni homoni ambayo inaruhusu glukosi iingie kwenye seli. Bila insulin sukari itabaki nyingi kwenye damu haitaingia kwenye seli.
Ukiwa na usugu wa insulin inamaanisha kuwa sukari iliyopo kwenye damu inakuwa ngumu sana kuingia kwenye damu na hivyo nyingi inabaki kwenye damu na kubadilishwa kuwa mafuta.
Kuwa na usugu wa insulin kunakuletea kitambi na uzito mkubwa. Usipotibu inakuja kuleta kisukari, presha, magonjwa ya moyo nk.
Usugu wa insulin unakuja kwa sababu ya kuwa na insulin nyingi kwenye damu muda mwingi na uwepo wa mafuta yanayoziba vipokea taarifa vya seli.
Kila unapokula, sio sukari tu, kila kitu kinapoingia mwilini kinahamasisha insulin kuingia kwenye damu.
Nikisema kila kitu namaanisha vyote. Hata kama ukila punje mbili za karanga, kuna kiwango fulani cha insulin kinazalishwa kuingia kwenye damu. Wengi wanafahamu ukila sukari tu ndio inapandisha insulin.
Hata hivyo kuna tofuati kubwa sana kati ya vyakula vyenye wanga na vyakula vyenye protein nyingi kwenye kupandisha insulin.
Mara nyingi imekuwa inapozungumziwa suala la vyakula vinavyopandisha insulin kwenye damu vimekuwa vinazungumziwa vyakula vya wanga na sukari.
Lakini insulin inahusika na vyakula vya protini na mafuta pia. Wanaolaumu wanga na sukari kuwa ndio vinaongeza kingo cha wanga wanakusukuma kula nyama na mafuta kwa wingi.
Bado huamini?
Hii hapa ni fact..
Protini pure, mafuta pure na sukari pure vyote vinapandisha insulin katika kiwango sawa sawa.[1] Yaani mtu aliyekula nyama ya ng’ombe, aliyekunywa mafuta na aliyekula sukari wote lao moja, insulin inapanda. Sio tu nyama ya ng’ombe hata samaki, maziwa, mayai pia.
Mayai hayana wanga lakini mafuta na protein vinaleta shida ya usugu wa insulin ambao utakusumbua sana kwenye kupunguza uzito na kitambi.
Shida ya usugu wa insulin inakuja pale utakapokula chakula chenye wanga. Hata kama kuna wanga kidogo sana sukari haiingii kwenye damu inabaki kwenye damu inabadilishwa kuwa mafuta.
Tuchukulie umekula asubuhi mayai, hapo umepandisha usugu wa insulin mara mbili kwa siku hiyo. Baadaye ukila chakula kingine chochote chenye wanga hata kama kina wanga kidogo sana sukari haiingii kwenye seli kwa namna inayotakiwa inabadilishwa kuwa mafuta.
Ili ufanikiwe kwa mtindo huu itakupasa usile kabisa wanga yaani ufanye ketogenic diet. Ni ile aina ya diet ambayo unakula mafuta mengi, protein kiasi na wanga kidogo sana chini ya asilimia 10. Hapo utawini lakini sio milele.
Ili mpango uwe mzuri milele lazima usiwe na madhara kwenye afya yako. Aina hii ya diet sio salama kiafya kwa muda mrefu.
Madhara yake ni haya miongoni mwa mengi
- Magonjwa ya moyo na mishipa ya damu
- Upungufu wa virutubisho ambao utakulazimu uishi kwa kutumia vidonge vya suppliments
- Upungufu wa nyuzilishe
- Kuongezeka kwa hatari ya kupata na kufa kwa saratani
- Inapunguza uwezo wa kukumbuka
Kolestro inayotokana na chakula kama mayai inaathiri uwezo wa ubongo ‘akili’, kumbukumbu na kuharakisha kuchakaa kwa ubongo kwa ujumla. Matokeo haya yanatokea kwa kula kolestro kuanzia 80mg ambazo ni sawa na kula nusu yai.[2]
Kupunguza uzito milele ni kupunguza uzito wakati huo ukifurahia tunu ya afya njema. Sio unapunguza uzito baadaye unakuwa na magonjwa sugu kwa sababu umepunguza kwa kula nyama na mayai.
- Udhaifu wa mwili
- Kukosa choo
- Maumivu ya kichwa
Tena kwa mayai ya kuku wa kisasa ndio kabisa unakuna na sumu inaitwa Phthalates.
Hii ni aina ya plastiki inayosababisha uzito mkubwa na kitambi; chanzo chake ni vyakula vya wanyama[3] kama nyama, maziwa ya wanyama (kama yamekamuliwa na mashine.. mambo ya wazungu huko), mayai ya kuku[4] na nyama ya kuku yenyewe.
Ukila kachumbari na mayai, madhara yanapungua sio sawa na alieyekula mayai pekee yake. Ukila mayai ya kuchemsha ni afadhali kuliko ya kukaanga kwa mafuta.
Afadhali haimaanishi ni bora. Inatumika unapochagua ikiwa itakulazimu.
Lakini,
Ili kuwa na matokeo mazuri zaidi ya muda mrefu ya kupunguza uzito mkubwa na kitambi mayai yawe ya kuku wa kisasa au ya kienyeji sio mazuri kuyatumia mara kwa mara kwa sababu yatakuchelewesha kufikia lengo.
Cha muhimu,
Kwenye kupunguza uzito milele ninachosisitiza ni mtindo bora wa maisha. Kile ambacho unakifanya mara kwa mara kila siku ndio ambacho kinakujenga au kinakubomoa.
Ikiwa utakuwa mtu wa kula mayai kila siku unajiharibu. Ikiwa mayai unakutana nayo mara moja moja hayaweza kukuletea shida.
Kama bado upo katika pambano la kupunguza uzito kiasi fulani au kuondoa kitambi nashauri mayai achana nayo yanakurudisha nyuma.
[1] Nuttall FQ, Mooradian AD, Gannon MC, Billington C, Krezowski P. Effect of protein ingestion on the glucose and insulin response to a standardized oral glucose load. Diabetes Care. 1984;7(5):465–70.
[2] Agricultural Research Service, United States Department of Agriculture. Basic report: 01123, egg, whole, raw, fresh. National Nutrient Database for Standard Reference 1. Published April 2018. Available at: https://ndb.nal.usda.gov/ndb/foods/show/01123. Accessed April 17, 2019.
[3] Ji K, Lim Kho Y, Park Y, Choi K. Influence of a five-day vegetarian diet on urinary levels of antibiotics and phthalate metabolites: a pilot study with “Temple Stay” participants. Environ Res. 2010;110(4):375–82.
[4] Colacino JA, Harris TR, Schecter A. Dietary intake is associated with phthalate body burden in a nationally representative sample. Environ Health Perspect. 2010;118(7):998–1003.