Faida, Madhara na Mbadala wa ASPRIN Kwa Magonjwa ya Moyo

Salicylic acid ni kiambata muhimu zaidi kwenye aspin. Imetumika kwa mamia ya miaka kwa ajili ya kuzima mioto ‘anti-inflamatory’ na kutuliza maumivu kwa wakati mmoja.

Historia inaonesha Hippocrates (tabibu mhenga wa kiyunani aliyeishi Kabla ya Kristo) alitumia salicylic acid kutoka kwenye magome ya mti wa willow kutibu homa na maumivu wakati wa kujifungua.

Toka mwaka 1899 huenda hadi leo, asprin ilitangazwa kuwa dawa inayotumika zaidi duniani. Mojawapo ya sababu inayoifanya dawa hii kuwa maarufu licha ya kuwepo kwa dawa nyingine za kutuliza maumivu ni kuwa asprin inatumika kusafisha damu ‘blood thinner’.

Kwahiyi mamilioni ya watu duniani hutumia aspein kila siku kwa ajili ya kujikinga au kutibu magonjwa ya moyo.

Mwaka 1970 utafiti ulifanyika kutazama kama kweli asprin inasaidia damu isigande. Matokeo yake ilikuwa kweli..

Kama matokeo ya damu kutoganda, inapunguza hatari ya kupata magonjwa ya moyo yanayotokana na damu kuganda kwenye mishipa midogo ya damu kwenye moyo.

Ndio maana leo mamilioni ya watu duniani wanaishi wakitumia dozi ndogo ili kujikinga na magonjwa ya moyo na kiharusi hasa wenye historia ya magonjwa hayo.

Lakini.. kuna madhara yake!

Asprin inapunguza hatari ya magonjwa ya moyo na kiharusi kwa watu ambao wanahistoria ya kuwa na magonjwa hayo kwa asilimia 2.5%. 

Madhara yake inasababisha damu kuvuja kwenye ubongo na kusababisha kulazwa au kufa kwa asilimia 0.4% y watumiaji. 

Ukiangalia faida ni kubwa kuliko hasara. 

Kwa ambao hawana historia ya magonjwa hayo bila kujali umri, matumizi ya asprin kila siku yanapunguza hatari ya kupata magonjwa ya moyo na kiharusi kwa asilimia 0.07%.

Kwa hawa ukilinganisha faida na hasara, hasara ni kubwa.

Mbadala wa Asprin

Tafiti zinaonesha kwamba hata ugonjwa wa moyo ambao umeendelea sana kuwa mbaya unaweza ukapona kwa chakula hai. Hii ni tiba rahisi sana yenye ufanisi mkubwa.

Chakula hai kinajumuisha mbegu nzima, matunda, mbogamboga, njugu na jamii ya kunde. Inakwenda sambamba na kuacha matumizi ya nyama, maziwa, mayai na samaki.

Kemikali iliyomo kwenye asprini ‘salicylic acid inpatiaka kwa asili kwenye chakula hai. Hivyo huna haja ya kula dawa kila siku hasa kama huna historia ya kupata magonjwa ya mishipa ya damu au magonjwa ya moyo.

Kula chakula hai utapata dozi ya asprini inayokutosha kukulinda dhidi ya magonjwa ya moyo na kiharusi.

NB: Nimetoa elimu kwa ajili ya uelewa wa jumla. Maamuzi ya matibabu na matokeo yake ni kati yako na daktari wako.

0 0 votes
Article Rating
Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Share
Scroll to Top