Punyeto Inasababisha UGUMBA?

Punyeto ni kitendo cha kusisimua kiungo cha uzazi kwa kutumia kitu tofauti na kiungo cha uzazi kwa lengo la kujiridhisha hisia za ngono.

Ikiwa itafanyika mara kwa mara na ikawa ni tabia kitendo hiki kinaleta madhara kwa wanaume na wanawake.

Madhara yake ni pamoja na kukupunguzia uwezo wa kufurahia ngono katika hali ya kawaida. Kwa mwanamke unakuwa hauwezi kupata msisimko wa kingono kirahisi na hivyo inakuwa sio rahisi kufika kileleni.

Kwa mwanaume, unapunguza uimara wa misuli ya uume na kupunguza uwezo wa kushiriki ngono kiasi cha kumridhisha mwenzi wako ipasavyo.

Kama ilivyo kwa tabia zingine hatarishi inawezekana unafanya kitendo hiki kwa muda mrefu lakini bado hujapata madhara, na ukajiona kuwa ni kitendo salama.. hapana!

Kuendesha gari kwa kasi kubwa kama 180kpm ni hatari sana. Ikiwa utaendesha kwa spidi hiyo na ukafika salama haimaanishi kuwa tabia hiyo nzuri Mshukuru Mungu kuwa amekulinda hadi sasa kukuepusha na madhara.

Chukua fursa hii, kujirekebisha! Kama usingekuwa unafanya kitendo hicho huenda ungekuwa bora zaidi kuliko ulivyo kwa sasa.

Punyeto Inasababisha Ugumba Kwa Wanawake?

Kitendo cha punyeto hakisababishi ugumba moja wa moja kwa wanawake.

Japokuwa, kulingana na namna mwanamke anavyofanya kitendo hicho hasa vitu anavyotumia vinaweza kuwa sio salama vikaharibu via vya uzazi au kupelekea kupata maambukizi kwenye mfumo wa uzazi ‘PID’ ambayo yakasababisha ugumba. 

Lakini moja kwa moja kitendo chenyewe hakisababishi ugumba.

Punyeto Inasababisha Ugumba Kwa Wanaume?

Punyeto kwa wanaume inaathiri zaidi misuli ya uume  na mfumo wa fahamu wa mwanaume. Haiathiri moja kwa moja kiwanda cha kuzalisha mbegu za uzazi.

Mbegu za uzazi zinazaliwa kila siku, kama malighafi zipo. Hata kama ziliharibiwa baada ya miezi 2 hadi 3 zinakuwa zimekomaa zingine.

Ukiacha leo punyeto, ukala vizuri, ukaacha unywaji na uvitaji, ukafanya mazoezi mbegu zinazalishwa za kutosha. Kufikia miezi mitatu tayari unazalisha vizuri.

Hata hivyo,

Wengi wenye tabia ya kujichua huwa wanakuwa na mazoezi mabaya mengine kama lishe duni, hawafanyi mazoezi na wengine ni wavutaji na watumiaji wa pombe.

Tabia hizi zinaongeza madhara zaidi hata kupelekea UGUMBA!

Jifunze jinsi ya kutibu madhara mengine ya punyeti kwa kubofya hapa

0 0 votes
Article Rating
Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Share
Scroll to Top