Umuhimu wa Kachumbari ‘Salad’ Kwenye Chakula

Kwanini ni Muhimu Kuongeza Chakula Kibichi (Saladi/Kachumbari) Kwenye Chakula Chako?

Ili upate faida za chakula unachokula iwe ni kwa ajili ya kukinga ugonjwa, kutibu ugonjwa, kupunguza uzito au kujenga mwili au faida nyingine yeyote ni lazima chakula hicho kimeng’enywe, kisharabiwe na kiingie kwenye seli ili kifanye kazi iliyokusudiwa.

Bahati mbaya ni kwamba sehemu kubwa ya watu wanataka kutumia chakula kama tiba au kufikia lengo lao wanakuwa tayari miili imechoka kiasi kwamba hata vimeng’enya vyenyewe vya kukivunja vunja chakula ili kiweze kusharabiwa havina nguvu au viko vichache. Kwahiyo licha ya kula kwa bidii chakula sahihi lakini bado matokeo ni haba.

Usiingie kwenye huu mtego wa kusema kuwa umejitahidi sana kula inavyotakiwa lakini huoni matokeo. Fahamu jinsi unavyoweza kutumia chakula kibichi kuboresha tiba lishe unayofanya.

Chakula kibichi kimebeba vimeng’enya vyake. Kinakuwa na dawa zake za kukimng’enya chakula unachokula. Kwahiyo mwili haupati kazi kubwa ya kuvimeng’enya na hivyo ni rahisi sana kutunza nguvu ya mwili na kupata virutubisho vyote katika chakula maana mmeng’enyo wake ni rahisi sana. Ni tofauti na chakula ambacho kimepikwa sehemu kubwa ya vimeng’enya kama sio vyote vinakuwa vimeharibiwa na moto.

Chakula kilichopikwa hakina vimeng’enya kama ilivyo kwa vyakula vibichi. Hata jinsi vinavyoathiri mwili ni tofauti sana. Mfano kiazi kibichi na kiazi killichochemshwa ni tofauti. Mgonjwa wa kisukari anaweza akala kiazi kibichi wala kisimletee shida yoyote lakini kama atakula kiazi kilichochemshwa utaona sukari yake inapanda.

Kadri unavyopika zaidi chakula kinapoteza uhai wake na hata ubora wakeunapungua.

Vile vimeng’enya vya mmea ambavyo vingesidia kukimeng’enya chakula vikisaidiana na vimeng’enya vya mwili vinakuwa vimekufa. Baadhi ya vitamins, kemikali mmea, na madini yanakuwa yameharibiwa kwa moto na hivyo kinakuwa ni kama chakula kingine kabisa ambacho kinatakiwa kitendewe kwa namna tofauti.

Na hivyo…

Hata vile vilivyokuwa bora sana kabla ya kupikwa vinapopikwa huenda visifae kabisa kwa baadhi ya watu na hasa wenye magonjwa au lengo fulani la kiafya kama kupunguza uzito.

Mwili unamfumo wake wa ukaguzi kujua aina gani ya chakula iliyoingia, itoe dawa gani kukisaga na ichukue virutubisho kiasi gani kutoka katika kile chakula.

Baadhi ya nadharia zinasema kuwa mfumo wa chakula hutumia homoni ya ukaguza inayoitwa incretin hormone Ili kufanya ukaguzi katika vyakula. Homoni hii hukagua chakula kwa kutumia muunganiko wa madini katika chakula hicho.

Jinsi inavyofanya kazi ni ngumu sana, haijulikani vizuri lakini huwa inaangalia aina na muunganiko wa madini katika chakula hicho.

Nitatoa mfano wa kubuni ili unielewe vizuri, unapokula kiazi kitamu kibichi kinakuwa na madini mengi, homoni hii inatambua kuwa katika asili chakula cha aina hii inatakiwa kuja ikiwa na madini mengi yakiwemo nitrogen (N), phosphorus (P) na magnesium (Mg) katika mpangilio N-P-Mg.

Mfumo huu wa ukaguzi unapoangalia kwenye kiazi kilichoingia mwilini ikaona huu mpangilio wa madini unasema, “aliyekuja ni muungwana”, baada ya kumenge’enywa, mwili utachukua kile tu kinachohitajika kwa sababu inakitambua vizuri hiki chakula.

Kama mwilini sukari ipo ya kutosha mwili hautachukua tena sukari nyingi, kama sukari imepungua mwilini mwili utachukua sukari zaidi kutoka kwa huyu muungwana aliyekuja.

Lakini pale chakula kinapopikwa, tuseme umepika kiazi mpangilio wa haya madini unabadilika na madini mengine yanawezapotea kabisa katika harakati za upishi.

Mfano madini yale matatu katika kiazi yanawezakuwa P-N. Katika mpangilio kama huu mwili hautaweza kujua hicho chakula kilichokuja ni cha aina gani. Kwahiyo unaweza ukapata shida ya kujazana virutubisho kama sukari kwenye damu au virutubisho vingine katika chakula ukavikosa kwa sababu mwili haujatambua.

(mfano huo hapo juu nimebuni ili unielewe, haitokei hivyo kwenye kiazi)

Mwili unapochanganyikiwa na kushindwa cha kuamua kunatokea kelele na mgogoro ambao unatafsiriwa kama magonjwa. Utasikia mtu anashida ya kisukari, shinikizo la juu la damu, uchovu wa mara kwa mara, upungufu wa vitamin na madini.

Unapokuwa mgonjwa au unataka kufikia lengo Fulani katika afya yako, jitahidi kwa sehemu kubwa inavyowezekana kula vyakula ambavyo havijapikwa. Kama ni lazima kupika visipikwe kwa muda mrefu wala visikangwe kwa mafuta badala yake unawezakutumia maji kukaanga au ukavukisha.

Kuna namna ya kufanya mwili umeng’enye na kutumia kwa busara chakula lilichokufa (kilichopikwa). Unapokuwa unakula chakula kibichi pamoja na kile kilichopikwa vile vimeng’enya katika chakula kibichi vinasaidia kukisaga vizuri hiki chakula kilichokufa na pia kuusaidia mfumo wa uchunguzi wa mwili kujua cha kufanya punde chakula hiki kinapofika hatua ya kusharabiwa.

Mmmh! Hebu subiri..!

kama utakuwa umenielewa maana ninayosema utaanza kula kile kibichi kabla ya kile kilichopikwa. Wengi huwa wanakula kwanza halaf chakula kibichi (kama ni mbogamboga au matunda) wanakula mwisho wanasema wanashushia, hapa utakuwa unajidanganya.

Anza kabisa mwanzoni, ili hata kama ukiwa umeshiba tayari umekula kilichobora. Na tena bakuli la kachumbari liwe kubwa sio vijiko viwili vitatu.

Kiwango cha chini cha chakula kibichi unachokula kinatakiwa kuwa..

5 X Uzito wako (kg) =___gram.

Mfano, kama una kilo 60, kiwango cha chini kinatakiwa kiwe 5 X 60 = 300gram. Kwahiiyo..

Unatakiwa kula angalau gram 300 za mbogamboga mbichi. Kama una uzito mkubwa utatakiwa kula hiki chakula kibichi kingi zaidi kuliko mwenye uzito mdogo. Kama hauna mnzani jitendee kwa ukaarimu kula mengine.

Sijalenga kila ukitaka kula uwe unapima. Lakini utakapokuwa ndio unaanza unaweza ukapima kwenye mnzani wa jikoni ili uweze kujua kiasi kinachotakiwa kikoje usije ukajipunja. Ukishakuwa umezoea umepata uzoefu unaachana na mambo ya kupima unakuwa unaandaa tu kwa kukadiria.

Kwani lazima nile kachumbari kabla?

Yaani badala ya kuanza kula hiyo salad kabla nikala pamoja na chakula sitapata faida. Kama ni wali nikala wali na saladi. Inawezekana kabisa ukapata faida sawa na yule anayekula saladi kabla ya kuanza kula chakula kingine kilichopikwa.

Kama ni hivyo kwanini nasisitiza ni vema ukaanza na saladi kwanza kabla ya kuanza kula kile chakula kingine?

Ni rahisi sana kusema umeshiba baada ya kula chakula chako kabla hata hujaanza kula saladi.
Na kwa sababu hujazoea kula saladi unaweza kuiona hana radha nzuri na usihamasike kuila kwa sababu ulimi wako ukawa umenogewa na chakula hicho kingine
Hata wanyama wanaishi kwa kula nyama wanaafya njema kwa sababu wanakula mbichi. Umewahi kusikia simba anakula swala rosti? Au chui anakula punda milia wa kuchoma? Na wakati mwingine wanayama hawa kula majani kidogo kwa ajili ya kujitibu.

Binadamu asijaribu kula ng’ombe mbichi hata hivyo hatujaumbwa kula nyama ila mimea. Ikiwa unataka kula nyama hakikisha unakula pamoja na chakula kingine kibichi ili kusaidiaa kumeng’enywa na kusharabiwa kistaarabu.

KUMBUKA:

Sio kila chakula kinawezaliwa kibichi, vingine ni lazima uvipike ili upate faida zake, na vingine haviliki kabisa bila kupika. Ninachosisitiza hapa fahamu nafasi ya vyakula vibichi katika lishe na hasa pale inapotumika katika tiba au kufikia lengo fulani kiafya.

Faida za Kula kachumbari ‘saladi’ Kabla ya Chakula Kingine

Kachumbari au saladi ni mchanganyiko wa mbogamboga mbichi. Napendekeza ziwe angalau aina nne. Mbogamboga kama nyanya, karoti, tango, kitunguu maji, pili pili hoho, parachichi, kabeji nk zinaweza kutumia kutengeneza kachumbari.

Kachumbari inaweza kuliwa muda wowote unaopenda. Na imetumika kwa miaka mingi kama namna mojawapo ya kutibu mwili kwa haraka.

Kachumbari ina faida kibao tukianza kuzipanga faida zake zinatosha kuwa kitabu. Lakini kula kachumbari kabla ya kula chakula kingjne kuna faida zifuatazo:

  1. Kukifanya chakula kiwe hai

Sehemu kubwa ya chakula kilichopikwa kinakuwa kimepungukiwa na virutubisho maana vingine vinakuwa vimeharibiwa katika mchakato wa kupika. Unapoweka chakula kibichi kinarudisha uhai wa chakula kile kwa sehemu fulani.

  1. Inaongeza uwezo wa mwili kumeng’enya chakula

Vyakula vilivyopikwa vimeng’enya vyake vinakuwa vimeharibiwa na moto na mwili unatumia nguvu kubwa kukisaga chakula. Kachumbari ina vimeng’enya vyake bado viko hai kwahiyo vinasaidia katika umeng’enyaji.

  1. Inaupatia mwili nyuzilishe kirutubisho ambacho kwenye vyakula vingi kwa kisasa hakipo kwa kiasi cha kutosha.
  2. Inaupatia mwili virutubisho

Inakusaidia Usile Kwa Wingi Vyakula Vitakavyokudhuru

5 2 votes
Article Rating
Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Ayubu Faustine Magashi
Ayubu Faustine Magashi
28 September 2023 16:09

Kama ni elimu tu kwakweli tumeivuna.., Mungu akubariki sana na kukutangulia Dr. Nature.., Tunaamini, Tunaheshimu na tunaipenda sana huduma yako maana inayo matokeo yanayoonekana bila pingamizi kabisa.

Share
Scroll to Top