Utashangazwa! Faida 8 Za Kiafya Za Sea Moss ‘Mwani’ (#1 Ni Tiba Ya Goita Bila Upasuaji)

Faida 8 za Sea moss ‘Mwani’ Kiafya

Sea Moss au mwani

Mwani ni mojawapo ya mbogamboga zinazopatikana baharini. Ni mojawapo ya chakula hai chenye upekee wake. Kwa sababu ni chanzo bora salama zaidi cha kuaminika cha madini joto ‘iodine’.

Katika ulimwengu wetu leo, madini joto yamekuwa adimu sana kwenye udongo kwa sababu ya shughuli za kibinadamu na tabia ya nchi.

Madini joto ni muhimu sana katika utendaji wa tezi ya shingo ‘thyroid’. Tezi ya shingo huzalisha homoni ambazo ndio zinaendesha shughuli za mwili. Hata suala la kuongezeka Uzito au kupungua Uzito linasimamiwa na homoni za tezi ya shingo.

Tezi ya shingo ikikosa madini joto ya kutosha inapelekea kuvimba na kutengeneza ugonjwa unaitwa goita. Hii inakuja baada ya kupitia dalili nyingine ndogo ndogo ambazo zinakukera ila unaweza usijue kama ni kwa sababu ya iodine kupungua.

Ndio maana kwenye chumvi inaongezwa iodine ili kunusuru wanadamu na upungufu huu. Hata hivyo hatari ni kuwa matumizi makubwa ya chumvi yanakuletea uzee wa mapema, uzto mkubwa  na magonjwa kama presha.

Kutumia sea moss sio tu kwamba inakukinga usipate goita lakini zaidi sana inakukinga na saratani ya tezi ya shingo pia.

Chanzo salama bora kupata madini joto ni kupitia mbogamboga za baharini kama sea moss. Kumbuka kuwa sea moss sio mbogamboga pekee zinazoliwa zinazopatikana baharini. Zingine ni kama

  1. Nori
  2. Wakame
  3. Kelp
  4. Hiziki
  5. Dulse
  6. Arame

Faida Zingine Za Sea Moss Kiafya

Mbali na kuwezesha tezi ya shingo kufanya kazi yake, inakulinda na ugonjwa goita. Hata kama una ugonjwa wa goita tayari itakusaidia kupona.

Faida zingine za matumizi ya sea moss ni pamoja na;

  1. Madini

Sea moss Inakupatia madini mbalimbali ikiwa ni pamoja na

  • Iodine – kwa ajili ya utendaji kazi wa tezi ya thyroid na utendaji kazi wa mwili kwa ujumla.
  • Kalsiamu – Sea moss ina kalsiamu, ambayo ni muhimu kwa afya ya mifupa na meno, pamoja na kazi ya misuli na usafirishaji wa taarifa kwenye neva Kwenda mwili mzima.
  • Magnesiamu – Magnesiamu ni muhimu kwa kazi ya misuli na neva, udhibiti wa sukari mwilini, na afya ya mifupa.
  • Potasiamu- Sea moss ina wingi wa potasiamu, elektrolaiti inayosaidia kudhibiti usawa wa maji mwilini, misuli inapojikunja, kuondoa usugu wa insulin na mawasiliano ya  za neva za fahamu.
  • Vitamini-Sea moss ni chanzo cha vitamini mbalimbali, ikiwa ni pamoja na vitamini A, vitamini E, vitamini K, na baadhi ya vitamini B kama riboflavin (B2) na folate (B9).
  • Chuma – Sea moss ina chuma, ambacho ni muhimu kwa uzalishaji wa seli nyekundu za damu na usafirishaji wa oksijeni mwilini.
  • Zinki – Zinki ni muhimu kwa kazi ya kinga, uponyaji wa majeraha, na usanisi wa DNA.
  • Fosforasi – Sea moss ina fosforasi, ambayo ni muhimu kwa afya ya mifupa, uzalishaji wa nishati, na muundo wa seli.
  • Antioxidant – Sea moss ina antioxidants hivi ni viondoa sumu kama vitamini C na flavonoids, ambazo husaidia kulinda seli kutokana na uharibifu unaosababishwa na kemikali zururaji ‘free radicals’.
  • Nyuzilishe –  Hizi ni kama mafagio kwenye utumbo kuondoa sumu, kulisha bakteria wazuri na kutusaidia kuwa na uzito unaofaa.
  1. Kushusha presha ya damu[1]

Kutokana na uwiano wa madini yaliyomo kwenye sea moss inasaidia kuweka presha ya damu kwenye usawa.

  1. Tiba ya gastritis

Gastritis ni michubuko au mioto kwenye tumbo. Sea moss imeonekana kusaidia sana kwenye kutibu.

  1. Tiba ya maumivu ya kichwa
  2. Inatibu Endometriosis

Endometriosis ni ugonjwa mbaya sana unaosababisha ulemavu na kuharibu ubora wa Maisha kwa wanawake. Hata hivyo bado ni ugonjwa ambao mgonjwa anaweza akahangaika nao muda mrefu kabla daktari hajafahamu kuwa ni ugonjwa huo.

Mimi ni shahidi pia wakati nikifanya kazi hospital kuna wagonjwa kadhaa ambao walihangaika sana kabla ya kuja kugunduliwa kuwa walikuwa wanasumbuliwa na ugonjwa huu.

Dalili zake ni pamoja na maumivu ya tumbo, maumivu wakati wa tendo la ndoa, siku zinakuwa hazina mpangilio na damu inatoka nyingi sana na ugumba.

Ugonjwa huu unasababishwa na damu ya hedhi kupanda juu badala ya kutoka nje ‘retrograde menstration’. Na matokeo yake tishu za damu zinajipandikiza kwenye viungo vingine.

Endometriosis ni ugonjwa unaohusiana sana na homoni ya estrogen kuwa nyingi. Ukiitibu kwa upasuaji uwezekano wa kurudi tena ni hadi asilimia 50 ndani ya miaka 5.[2]

Vyakula vyenye phytoestrogen kama soya vinasaidia sana kukinga usipate endometriosis. Phytoestrogen inafanya kazi kinyume na estrogen ya mwili na hivyo inakupunguzia hatari ya kupata ugonjwa huu.

Mbogamboga za baharini kama sea moss zina aina fulani maalumu ya nyuzilishe na virutubisho ambayo havipatikani kwenye mimea ya nchi kavu. Ambavyo vina uwezo mkubwa sana wa kutibu endometriosis na saratani.

  1. Inabalance homoni za kike

Mbogamboga za baharini kama sea moss pamoja na soya vinamsaidia mwanamke kuwa na mizunguko mirefu yenye hedhi iliyotulia ya siku chache.

Inawezekana inafanya kazi kwa kuzuia uzalishwaji wa estrogen au kuharakakisha kuvunjwa kwake, au inazuai vipokea taarifa vya eastrogen.[3]

Kwa kutumia  ½ kiijiko cha chai kwa siku unaweza ukapunguza hadi 85% ya kiwango cha estrogen..

  1. Inapunguza dalili za sonona na msongo
  2. Kupandisha kinga ya mwili

Inapandisha kinga ya mwili na hivyo

  • Kupunguza au kukuepusha kabisa na allege za msimu kama mafua
  • Inazidisha mara nne uzalishwaji wa seli za kinga T-cells ambazo zinapambana sana na magonjwa ya virus.
  • Inaongeza anti-bodies (walinzi wa mwili) kuliko chanjo nyingi hasa kwa watu wazima[4]

Kiasi kinachotakiwa

Kwa siku unahitaji 150mcg ya iodine.

½ kijiko cha chai cha sea moss kwa siku inatosha kukupatia mahitaji ya iodine kwa siku.[5]

Imeandaliwa na Dr Nature

Simu/Whatsapp: +255767759137

 

Reference

[1] Hata Y, Nakajima K, Uchida J, Hidaka H, Nakano, T. linical Effects of Brown Seaweed, Undaria pinnatifida (wakame), on Blood Pressure in Hypertensive Subjects. Journal of Clinical Biochemistry and Nutrition Vol. 30 (2001) P 43-53.

[2] Berlanda N, Vercellini P, Fedele L. The outcomes of repeat surgery for recurrent symptomatic endometriosis. Curr Opin Obstet Gynecol. 2010 Aug;22(4):320-5.

[3] Teas J, Hurley TG, Hebert JR, Franke AA, Sepkovic DW, Kurzer MS. Dietary seaweed modifies estrogen and phytoestrogen metabolism in healthy postmenopausal women. J Nutr. 2009 May;139(5):939-44.

[4] Shan BE, Yoshida Y, Kuroda E, Yamashita U. Immunomodulating activity of seaweed extract on human lymphocytes in vitro. Int J Immunopharmacol. 1999 Jan;21(1):59-70.

[5] Teas J, Pino S, Critchley A, Braverman LE. Variability of iodine content in common commercially available edible seaweeds. Thyroid. 2004;14(10):836–41.

3.3 3 votes
Article Rating
Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Share
Scroll to Top