Njia ya KUPUNGUZA UZITO na KITAMBI Rahisi, Salama na Ufanisi 100% Ni Hii..

Hakuna Njia KUPUNGUZA UZITO na KITAMBI Rahisi, Salama na Yenye Ufanisi Kuliko Hii…

Najua umeshawahi kufanya program nyingi za kupunguza uzito/au kitambi..

Kama umewahi kufanya program ninayofundisha utakuwa shahidi..

Kama bado, utajuta kwanini hukuanza miezi 6 iliyopita..

Unaweza kupungua kwa kufanya mambo mengi mengine ni magumu, gharama kubwa na mengine yanaweza kugharimu afya yako..

Kama hujawahi kusikia kuna hizi

  • Kujinyima chakula.. hawa wanashinda njaa kwa kunywa juisi na matunda
  • kuna wale wanaokunywa dawa za kuharisha.. wakati nikiwa Mawenzi hospital nimewahi kumlaza mama miaka 36 nusu afe kwa kuharisha na kutapika baada ya kunywa dawa ya kupunguza tumbo
  • Kuna wale wanaokimbia kula wanga wanakula nyama, mayai, samaki na maziwa + mafuta kama huyo niliye-share na sisi yaliyomkuta
  • Kuna wanaoshinda gym kupambania asilimia 15% za uzito huku wakisahau wanachoweka mdomoni..

Wengine wanapungua ila wakiacha tu mazoezi uzito unarudi mara 2..

  • kuna ambao wanaenda Muhimbili kuwekewa baloon..
  • Kuna ambao wanashinda na mikanda ya kubana tumbo na kubana matumbo wakati wa kupiga picha..
  • Siku hizi kuna vidonge vya kinyesi, kwa ajili ya kuwasaidia watu kupungua..

Ipo kisayansi (usicheke).. inatumia kanuni ya kurudisha bakteria wazuri kwenye utumbo

  • Kuna ambao wanafanyiwa upasuaji kukata sehemu ya tumbo ili kupunguza kiwango cha chakula kinachoingia kwenye damu..

Aisee mambo ni mengi sana..

Unaweza hata ukachanganyikiwa na kuishia kukata tamaa hadi utakapokuja kugundua Dr Nature nawaelekeza watu njia mtelezo..

Mimi ni daktari wa binadamu (MD) ambaye nimejikita katika mtindo wa maisha..

Nimewasaidia wengi vibonge kufikia malengo yao bila kuhangaika na huku wakifurahia faida kibao kiafya..

Natumia ‘Chakula Hai’ na Easy Chopper’ kwa sehemu kubwa kufanya hivyo✅

Siwezi kubeza njia za wataalamu wenzangu katika kupambana na uzito mkubwa na kitambi..

Lakini..

Kama unatafuta njia ambayo ni rahisi salama na yenye ufanisi mkubwa kwa kudumu utahitaji kusikiliza ninachokufundisha..

Ni evidence based na imewasaidia wengi, inshallah itakusaidia pia.

Kupunguza uzito na kitambi milele unatakiwa kubadili mtindo wako wa maisha.. kwa sababu ndio chanzo..

Yaani kuondoa kulichosababisha uwe hivyo..

Sehemu kubwa kama 80% ni chakula! Ndio maana nafundisha

‘Chakula hai’

Hicho unaweza ukakitumia kupungua na kutunza matokeo hayo milele..

Easy chopper ni virutubisho ambavyo nimevitengeneza kukurahisishia uchome mafuta haraka wakati unajifunza lifestyle inayofaa kukupatia matokeo ya milele

sehemu nyingine inayobakia inachukuliwa na mazoezi, kulala usingizi wa kutosha nk.

Misheni yangu ni kukusaidia ufikie lengo lako, bila kuhangaika! Na inawezekana kabisa 100%

Shared with ❤️
Dr Nature

Share
Scroll to Top