Chai ya Mbegu za Maboga: Jinsi ya Kutengeneza na Umuhimu Kwa Anayenyonyesha

Chai ya MBEGU ZA MABOGA Kwa Mama Anayenyonyesha

Wamama wengi baada ya kujifungua wanakuwa katika kipindi cha

‘UBONGE’

Wananenepeana sana kwa sababu ya lishe mbovu ya mitori na supu za mama mkwe.

Wanaogopa kufanya program za kupungua kwa kuhofia maziwa.

Wengi wanaamini kula sana ndio kupata maziwa .. SIO SAWA..

Kupata maziwa ni KULA VIZURI..

Kama unafanya program yangu y kupunguza uzito katika kipindi cha kunyonyesha natarajia unapata maziwa mengi.

Lakini kama maziwa ni kidogo au ni mepesi tumia hii chai

Mbegu za maboga ni zina virutubisho vingi sana ikiwemo madini ya zink, magnesium, vitamin C, calcium, mafuta mazuri, protini

Zinasaidia sana kwenye kuzalisha maziwa mengi na kuyafanya yawe bora.

Ukizitumia kwa wingi utaona matunda kwenye maziwa yako..

Utaona pia hata mtoto atakuwa analala vizuri huenda mikesha ikapungua na ukuaji wa mtoto unaongezeka.

JINSI YA KUTENGENEZA

Nunua mbegu za maboga usage mwenyewe (unga wa mbegu za maboga uliosagwa ni ghali).

Osha vizuri zianike zikauke, halaf kaanga kisha.. Saga kwenye blenda au food procesor kisha chuja.. tayari umepata unga utunze kwenye chombo kisafi.

Unaweza ukautumia kwenye chai, tumia chai ya viungo kisha chota kijiko 1 au viwili koroga kwenye kikombe, ina radha nzuri mno!

Pia unaweza ukautumia kwenye .. Uji, maji, juisi, smoothie, mboga, chakula kingine, unaweza ukalamba.. vyovyote vile cha muhimu ziingie tumboni..

So usiogope kufanya program y kupunguza uzito kiafya kwa kuwa unanyonyesha.

Zingatia neno ‘kiafya’ sio unaanza kushinda njaa au unashindia.. Juisi ili upungue wakati unanyonyesha, kwanza njaa ya kunyonyesha haitakuacha ulale😂

Unaweza ukajiunga na group langu la whatapp ujifunze tips zaidi:

Group la Permanent Weightloss: https://chat.whatsapp.com/EiBLnokVR9H3v4JV1yf1i5

Nitawaambia siku nyingine umuhimu kwa wanaume..

Shared with ❤️
Dr Nature

Share
Scroll to Top