Chakula Hai – Mwongozo wa Tiba Lishe (+Ratiba ya Siku 7)

Mwongozo wa lishe haujawahi kuwa rahisi kama hivi..

Maelfu ya watu wenye magonjwa na malengo mbalimbali ya kiafya wamefuata namna hii rahisi ya kula na matokeo yake ni kama muujiza!

Mbali na kutibu mamia ya magonjwa ambayo vinginevyo hayatibiki au yangekughalimu mamilion kutibu, aina hii ya kula itakusaidia kuongeza kasi ya mwili kuchoma mafuta, kuondoa njaa za mara kwa mara na hivyo kupunguza uzito mkubwa na kitambi kirahisi.

ASUBUHI

(Saa 10 alfajiri na saa 6 mchana)

Kula matunda aina 3-4. Mfano; maembe, machungwa, ndizi, tikiti maji, papai, nanasi, parachichi, chenza, zabibu, nk

Changanya matunda, katakata kula hadi ushibe. Ukisikia njaa tena kabla ya saa 6 mchana kula matunda mengine.

MCHANA

Andaa bakuli kubwa la kachumbari ya nyanya, karoti, tango, kitunguu maji, kabeji, pilipili hoho na parachichi au nazi ulizokwangua. Ziwe nyingi kula kabla ya chakula cha mchana.

Kwenye kachumbari unaruhusiwa kuweka LIMAU, NDIMU au VINEGAR.

TAHADHARI: Usiweke chumvi, ukitaka kuweka weka kwa mbali sana wakati ukijifunza kuiacha.

Chakula kingine utakachokula baada ya kula kachumbari kiwe ni chakula kinachotokana na mimea mbegu nzima na mbogamboga. Namaanisha kama ni nafaka ziwe nafaka ambazo hazijakobolewa. Mbegu zingine ni jamii ya kunde kama maharage, choroko, dengu, mbaazi, nk. Chakula hiki kiandaliwe bila mafuta mengi wala chumvi nyingi.

…Hakuna haja ya kukaa muda fulani, baada ya kula kachumbari kabla hujala chakula kingine….

Mfano:

Kula kuchumbari, ukimaliza kula wali wa maua na njugu mawe kama mboga. Unapopika tumia mafuta kidogo na chumvi ya kuonjeka.

JIONI

Chakula cha jioni fanya kama ulivyofanya mchana (sio lazima chakula ulichokula mchana). Yaani kula kwanza kachumbari kisha chakula kingine ambacho kimetokana na mimea cha asili.

Chakula cha jioni kula kabla saa 2 haijafika, kula mapema inavyowezekana.

Chakula kingine:

Hivi unaweza ukala muda wowote unataka

Jamii ya karanga kama karanga, korosho, almond, flax seeds nk, tumia mbegu zilizojaa kwenye kiganja kimoja mbichi baada ya kulowekwa.

Chai ya viungo kama tangawizi, manjano, karafuu, mchaichai, nk

EPUKA KULA‼️

Maziwa, nyama, mayai, samaki na mazao yake yote Vyakula vilivyowekwa kwenye packet na vilivyosindikwa viwandani.

Vyakula vilivyochakatwa kama sukari na nafaka zilizokobolewa.

Chakua hai

Pata Ratiba ya Chakula Hai Ya Siku 7

Hii itakusaidia kuona kwa mfano, jinsi ambavyo unaweza ukapangilia milo yako kwa siku 7 kuanzia leo!

Lipia Tshs 5,000 tu kisha nitakutumia kwenye Whatsapp au Email yako!

Njia ya malipo:

MPESA 0767759137 jina YUSUFU FILEMON

AU

Lipa namba ya Tigo 9933745 jina DR NATURE

  • Kama unalipia kutoka nje ya Tanzania wasiliana na mimi kupitia Whatsapp hiyo hapo chini nikupatie maelekezo

Ukishalipia, nitumie ujumbe wa mwamala wako Kwenye whatsapp yangu +255767759137

Kama ndani ya masaa 24 hujapata eBook yako nipigie simu kwa namba hiyo hiyo.

Mungu akubariki!

Wako,

Dr Nature | Healthy Lifetyle Coach

4.5 2 votes
Article Rating
Subscribe
Notify of
guest
3 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
trackback

[…] Chakula hai kinajumuisha mbegu nzima, matunda, mbogamboga, njugu na jamii ya kunde. Inakwenda sambamba na kuacha matumizi ya nyama, maziwa, mayai na samaki. […]

trackback

[…] Kama hufahamu chakula hai ni kipi maelekezo haya hapa BURE!! […]

trackback

[…] kama ilivyo vyakula hai vingine vinaufanya mwili uwe na afya njema kwa […]

Share
Scroll to Top