Chumvi Inanenepesha?

Chumvi Inanenepesha?

Kabla sijakuambia kwamba jibu ni NDIO..

Kumbuka kwamba 

1. siku hizi tunakula chumvi mara kumi (10) ya kiasi ambacho miili yetu imeumbwa kutumia.

2. Chumvi mojawapo ya vitu vinavyoleta uraibu wa chakula .. kama ilivyo mafuta na sukari..

Uhusiano wa chumvi na uzito mkubwa..

1. Inaongeza hamu ya kunywa vinywaji baridi kama soda bila wewe kujua..

Tafuti zinaonesha ukipunguz  an chumvi na hamu ya vinywaji baridi inapungua.

Na unajua ukinywa soda sana kitambi na uzito viko jirani na wewe

2. Inasababisha mwili kutunza maji zaidi na hivyo inaharibu ‘bioimpendence measurement’ ya mwili. Ilipo chumvi ndipo maji yanapoenda.

3. Chumvi nyingi inasababisha uzito wa mwili kuhama kutoka kwenye ‘lean mass’ misuli, mifupa na viungo vingine kuwa mafuta zaidi

Kadri unavyokuwa na chumvi nyingi mwilini, ndivyo utakavyotunza mafuta mengi hasa ya tumboni (kitambi)

4. Chumvi nyingi inahamasisha homoni ya ghrelin kufanya kazi. Hii hi homoni inayokufanya ujisikie njaa inataka kukuua😂

Ikifanya kazi ndio unasikia tumbo ni kama linauma njaa

Kwahiyo..

Unakuwa unatamani kula zaidi zaidi.. 

Ukila vibaya mfano kwa kuweka chumvi nyingi unaweza ukadhani mwili unahitaji zaidi nishati kumbe umeharibu ile mifumo asili ya mwili ya kukupunguzia njaa ambazo hahitajiki..

Hayo mambo manne yanakufanya unone kama ukila chumvi nyingi..

Hivyo..

– usike chumvi kwenye salad (kachumbari)

– usiongeze chumvi mezani baada ya chakula kuwa kimeiva

– epuka kununua bidhaa ambazo zimeongezwa chumvi

– Pika chakula chako mwenyewe bila kuweka chumvi nyingi

– Anza kujizoeza kujipunguzia chumvi 

Ukifanya hivyo..

Itakusaidia kupunguza uzito na kitambi na kujikinga usinenepe tena au kujenga kitambi kingine

Shared with ❤️ 

Dr Nature

Share
Scroll to Top