Mjamzito Anaruhusiwa Kufanya Diet?

Mjamzito Anaruhusiwa Kufanya Diet?

Kama upo hai basi lazima unakula.. hiyo kula yenyewe ndio diet😂😂

Ile namna ambayo unapangilia chakula chako ndio ‘diet’ kwa kiingereza.

Ilivyozoeleka ukisema diet hasa sisj wabongo tunamaanisha ‘special diet’

Special diet ni ule mpangilio maalumu wa chakula kulingana na mahitaji ya watu maalumu ama kwa sababu ya ugonjwa au lengo fulani..

Mfano, mwenye kisukari anakuwa na special diet inayolenga kutibu au kusaidia ku-control sukari yake

Wenye kitambi na uzito mkubwa Wanakuwa na special diet ili kuwasaidia mwili uchome mafuta.

Akina mama K nao wana diet yao ambayo kwao inalenga kumsidia mtoto kuumbika vizuri na kukua vizuri.

Je, vipi kama mama K anauzito mkubwa, afanye diet ya wenye kitambi kama ninavyofundisha?

Kiwango cha mafuta ya ziada kwa mjamzito .. yaani mama K akiwa ‘obese’ ni hatari kwake na mtoto wake.

Kwake inaweza kumsababishia akapata kisukari cha mimba, presha na kifafa cha mimba au hata mimba kuharibika.

Wakati wa kujifungua inakuwa ni heka heka

Inaongeza hatari ya kujifungua kwa upasuaji.

Pia mama akiwa na uzito mkubwa na kitambi wakati wa ujauzito anawez akamrithisha mwanaye ‘epigenetics’ za uzito mkubwa.

Kwahiyo mtoto katika maisha yake atakuwa katika hatari ya kuwa na uzito mkubwa na kitambi..

Kuliko wengine na hatakupunguza uzito kwao inakuwa ni ngumu zaidi kuliko wengine (japo inawezekana).

Hivyo ni muhimu sana kwa mwanamke kabla ya kubeba mimba punguza uzito ondoa kitambi..

Kama unashindwa mtafute Dr Nature ⁨0767 759 137⁩ au jiunge na group lake https://chat.whatsapp.com/EiBLnokVR9H3v4JV1yf1i5

Wengi wetu hatuna maandalizi ya kubeba mimba.. inakuwaga tu ‘babe siku zangu sizioni’😂

Ikitokea tayari ni mjamzito na bado unauzito mkubwa

NB: Ni kawaida na ni muhimu kwa mama K kuongezeka uzito wakati wa ujauzito..

Hapa nazungumzia uzito mkubwa hata kabla ya kupata ujauzito.

Ukijikuta katika hali kama hiyo…

MJAMZITO USIFANYE ‘EXTREMES’ ZA DIET!

Soma tena hayo maandishi makubwa..

Namaanish usije ukaanza yale mambo ya kushindia juisi, mara umefunga siku tatu.. unajinyima chakula ila upungue HAPANA!

Wakati huu ndio muda wa kula chakula hai yaani diet ambayo kwa sehemu kubwa imetokana na mimea katika uasili wake..

Chakula hai ni …Chakula ambayo kimethibitika kisayansi kuwa kinasidia kuupatia mwili virutubisho, kuukarabati na kutibu magonjwa..

Ni chakula ambayo kwa asili binadamu wote wanatakiwa wale.. kutakuwa na msisitizo wa aina na mpangilio wa hivyo vyakula lakini ni CHAKULA HAI

Wajawazito watumie kwa wingi diet yenye wingi wa MATUNDA, MBOGAMBOGA, NAFAKA NZIMA, JAMII YA KUNDE na NJUGU yaani jamii ya karanga..

Waache kabisa matumizi ya sukari, nafaka zilizokobolewa, pombe, mafuta mengi, chumvi nyingi, vyakula vilivyokangwa na Vyakula vya makopo⚠️

Wale zaidi vyakula asili kwa wingi ambavyo vimetokana na mimea.

Vinasaidia sio tu kukuepusha na kuendelea kuongezeka uzito lakinj kumlinda mtoto akue vizuri na kumpunguzia madhara ya uzito wako mkubwa.

Kwahiyo mama K pia anaweza akala kachumbari ✅ ya matunda na mbogamboga pia.

Kwa siku ukipata big salad ya matunda mara moja na big salad ya mbogambog mara moja.. itakusaidia sana!

Chagua tu yale unayoweza kula vizuri usije ukatapika mama😂

Shared with ❤️
Dr Nature

Share
Scroll to Top