Lipoma Ni Nini Na Inahusianaje Na Uzito Mkubwa

Lipoma ni nini na inahusianaje na uzito mkubwa?

Lipoma ni uvimbe unaotokea kwenye seli za mafuta kwa kawaida unatokea chini ya ngozi.

Uvimbe huu huwa sio saratani na huwa hauna maumivu.

Aina hii ya uvimbe huwa haileti madhara kwenye afya mtu anaweza kuishi nayo kwa muda

Isipokuwa kama uvimbe utakuwa mkubwa sana (kulingana pia na mahali ulipo) unaweza ukasababisha pressure kwenye tishu zinazouzunguka na kusabbisha maumivu.

Mara zote huwa sio saratani hata hivyo mara chache sanaaa vinawezakubadilika na kuwa saratani ‘liposarcoma’ ni rare sana

Nini kinasababisha lipoma?

Hakuna kitu kimoja kinachofahamika, ila kuna vitu mbalimbali vinavyoweza kuongeza uwezekano wa hizi seli za mafuta kukua kw kasi na kujifungia kwenye capsule..

Sabbabu kubwa ni pale ambapo mchakato wa shughuli za mwili unaathiriwa ‘metabolic factors’

Mfano, unapokuwa na UZITO MKUBWA … mambo mengi sana hubadilika ikiwemo jinsi mwili unavyofanya kazi zake na pia mfumo wa homoni unabadilika..

Na hivyo unakuwa kwenye hatari ya kupata magonjwa mengi ikiwemo uvimbe mbalimbali kama lipoma, fibroids, PCOS nk

Vihatarishi vingine ni umri na kurithi..

Matibabu:

Kama ni kadogo hakukusumbui unaweza ukakaacha tu .. ukaona kanaendeleaje..

Kama ni kubwa inakusumbua, yafuatayo yanaweza kufanyika

  1. Upasuaji kuukata uvimbe
  2. Upasuaji wa tundu dogo kuyafyonza mafuta ‘liposuction’
  3. Sindano za steroids kupunguza ukubwa wa uvimbe hasa kama ni mkubwa na upo eneo ambalo upasuaji unawezakuwa changamoto

Ushauri wangu:

Pamoja na kufuata taratibu za daktari wako hospitali, fanya haya ambayo sitegemei utayapata hospitali..

‘KULA CHAKULA HAI’

Kitakusaidia kusolve issue ya metabolism ambayo inaweza kuwa imesababisha uvimbe kutokea

Kama unauzito mkubwa

‘PUNGUZA UZITO NA KITAMBI’

Fuata program ya kupunguza uziti kiafya kama ninayofundiasha, itakusaidia kuondoa mafuta ya ziada mwilini.

Shared with ❤️
Dr Nature

0 0 votes
Article Rating
Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Share
Scroll to Top