Diet ya Nyama ‘KETOGENIC’ Ni Ergolytic?

Mwezi September 2023 Brother mmoja miaka 32 anaitwa Nasibu Jr alijiunga na program yangu ya PERMANENT WEIGHTLOSS.

Akaifanya kwa bidii kwa wiki 5. Kisha jioni moja ananipigia simu kunishukuru.

Amekuwa akipambana na uzito mkubwa kwa miaka miwili.

Uzito wake uliongezeka hadi kufikia 98kg lengo lake afike 65kg.

Katika harakati zake za kutafuta mbinu alikuwa kwenye program ya diet inaitwa KETOGENIC DIET

Kama huifaham hii ni diet ambayo asilimia 70 ya kalori unazipata kwa kula mafuta, asilimia 20 kutoka kwenye protini na chini ya asilimia 10 kutoka kwenye wanga.

Yaani ‘Low carb high fat diet’.

Unapaswa kuepuka kabisa wanga ikiwemo matunda na ule zaidi nyama, mayai, maziwa, samaki na jamii ya karanga.

Hata mbogamboga zenye wanga kama karoti, viazi au nafaka haziruhusiwi.

Moja ya kitu ambacho Nasibu alinambia ni kuwa kwa kufuata hiyo lishe alipungua kutoka 98 hadi 80 kwa miezi 4.

LAKINI

Kilichokuwa kinamsumbua ni KUKOSA NGUVU

Hata mchezo wa mpira wa miguu aliokuwa anapenda kucheza kila jioni. Ilibidi aahirishe kwanza.

Maana wakufunzi wake walimwelekeza kuwa hiyo ni hali ya kawaida kwa sababu ya mabadiliko ya mwili itaisha.

Lakini hali haikuisha.

Kwa sababu kula nyama, mayai na maziwa ni GHARAMA zaidi kuliko namna nyingine ya kula alijikuta anaacha hiyo diet kwa sababu hakuweza kuiendeleza.

Kidogo kidogo alianza kuongezeka tena hadi anajiunga na PERMANENT WEIGHTLOSS alikuwa na kilo 102kg.

Kwa wiki 5 alizofanya CHAKULA HAI alipunguza kilo 3 lakini alinambia anajisikia vizuri kama amepunguza kilo 20.

Anajisikia kuwa na nguvu. Na chakula hai ni rahisi kukitekeleza kama familia na kuendelea maisha yote.

Nikakumbuka kuna siku nikasoma report ya International Society of Sports Nutrition hiki ni chama cha kimataifa cha lishe ya wanamichezo..

Wakasema..

Keyogenic diet hiyo diet ya mafuta kwa wingi ni ERGOLYTIC.

Ergolytic maana yake ni kinyume cha ERGOGENIC. Kitu ambacho ni ergolytic kinaharibu uwezo wa mwanamichezo kufanya vizuri.

Kinapunguza nguvu, kasi na uwezo wa kuvumilia katika michezo na hivyo ndivyo ilivyo ketogenic diet.

Sio wazo zuri kufanya ketogenic diet kuwa lishe yako kwa ajili ya kupunguza uzito au kutunza afya yako.

Badala yake fanya chakula hai ni rahisi, salama na yenye ufanisi wa hali ya juu!

Dr Nature

0 0 votes
Article Rating
Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Share
Scroll to Top