Jinsi ya Kupunguza Kalori Bila Kujinyima Chakula

Jinsi ya Kupunguza Kalori Bila Kujinyima Chakula

Tabibu mmoja aliwahi kusema

‘’Aliyekula hadi akaugua inatakiwa kufunga hadi apone’’.

Ukiwa na kitambi au uzito mkubwa ni matokeo ya kulundikana kwa ziada ya chakula katika namna ya mafuta.

Kufunga ni salaha nzuri ya kukusaidia kuufanya mwili utumie hifadhi hiyo ya chakula iliyopo mwilini tayari.

Unapopambana na kupunguza uzito mkubwa na kitambi kwa wengi tunapambana na hamu ya kula mara kwa mara.

Unatamani kula mara kwa mara licha ya kuwa na ziada ya chakula kwa wingi kama mafuta.

Ushauri maarufu ni kuwa punguza kiasi unachokula.

Hamu ya kula inaendeshwa na nguvu ya asili ya mwili kama ilivyo kupumua. Unaweza ukajizuia kupumua kwa muda mfupi lakini baada ya muda utanyoosha mikono.

Ukipunguza kiasi cha kula kwa kujilazimisha hamu ya kula inaongezeka.

Utatumia nguvu kubwa sana kupambana na hii hali na haitakusaidia kwa muda mrefu kwa sababu itafika mahali utashindwa.

Hasara nyingine ni kuwa ukipunguza kiasi cha chakula kwa kujilazimisha unapoteza misuli na uimara wa mifupa kama hufanyi mazoezi.

Namna ambayo ni nzuri zaidi ni kufunga kwa masaa machache kila siku..

‘intermittent fasting’

Ni namna ya kufunga ambayo kila siku unakuwa na masaa kati ya 12 hadi 21 ambayo huli chochote.

Mfano:

Chakula cha jioni ukila saa 12 na cha asubuhi ukala saa 4 asubuhi unakuwa umekaa masaa 16 bila kula.

Kama ukila saa 1 usiku hadi kesho saa 2 asubuhi unakuwa umefunga masaa 11.

Namna hii ya kufunga unapata faida kama masaa uliyofunga yahusisha masaa ya giza (usiku).

Ukifanya hivyo inakusaidia kupunguza kiasi cha kalori kinachoingia mwilini hata bila kujinyima chakula.

Haiharibu misuli waka kupunguza uimara wa mifupa.

Inaweza kukusaidia kupunguza uzito hata kama huli chakula hai.

Ukifanya hivyo na huku unakula chakula hai, matokeo yake ni makubwa zaidi!

Dr Nature | +255767759137

0 0 votes
Article Rating
Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Share
Scroll to Top