Huu ndio ushauri wa kwanza utausikia kwa kila mtu (ila sio mimi)…
‘Ukitaka kupunguza uzito au kitambi fanya mazoezi’
Hata hivyo mazoezi yanachangia asilimia 15% na matokeo yake ni yanategemea vitu vingi ambavyo nataka nikueleze
Usinielewe vibaya.. mazoezi ni muhimu sana sio tu kwa ajili ya kuchoma mafuta bali kwa ajili ya kujenga afya kwa ujumla.
Ila kwenye suala la kuchoma mafuta yana nafasi kidogo ukilinganisha na mambo mengine kama chakula na usingizi.. ndio usingizi..
Kulala vizuri kunasaidia sana
Zingatia haya kuhusu mazoezi unapotaka kuchoma mafuta milele
- Aina ya mazoezi
Aina nyingi sana za mazoezi zinafaa.. ila chagua mazoezi ambayo unayafurahia… kama unayafurahia inaama utaweza kuyafanya kila siku bila kujiwekea visingizio
Kumbuka ili matokeo ya mazoezi yawe endelevu lazima ufanye mazoezi kila siku.. sasa kama unafanya mazoezi usiyapenda kwa kujilazimisha hutaenda mbali.
Kama unapenda kukimbi, kucheza mpira, kuendesha baiskeli, kuruka kamba, kutembea, nk fanya hayo kila siku
⚠️ kuna mazoezi ambayo hayakusaidii kuchoma mafuta kwa sababu ya matokeo yake baada ya mazoezi (utakula sana) mfano. Kuogelea
- Muda Mzuri Kufanya Mazoezi
Muda mzuri ni asubuhi kabla hujala.. tafiti zinaonesha kwamba ukifanya mazoezi asubuhi kabla hujala
Inaounguza store ya glycogen kwa 18% na hivyo kuanzisha mchakato wa mwili kuchoma mafuta zaidi kwa siku hiyo..
Wengi tunafanya mazoezi jioni. Huend isitusaidie kufikia malengo yetu.
Hata hivyo kama unafanya mazoezi kwa ajili ya lengo lingine tofauti na kuchoma mafuta inawezafaa
- Fanya kidogo kidogo kila siku
Ukifanya mazoezi mazito siku chache kwa wiki mfano ukatumi masaa 6 kufanya mazoezi kw siku 2 au 3 halaf ukaacha ukafanya tena wiki ijayo unaweza usipate faida kwenye kuchoma mafuta..
Kwa sababu kila siku mafuta yanatunzwa na unapaswa kuyachoma
Namna nzuri ya kufanya ni kufanya mazoezi kidogo kidogo kwa siku nyingi katika wiki angalau siku 5 kwa wiki..
Kwahiyo..
Kupata faida zote za mazowzi katika kuchoma mafuta ‘Chagua zoezi unalopenda, fanya kila siku asubuhi kabla hujala angalau siku 5 kwa wiki’
Shared with ❤️
Dr Nature