Mazoezi Yanayofaa Kupunguza Uzito Milele

Aina ya MAZOEZI Unayoweza Kufanya Ukapunguza Uzito Milele

Mtu kama akinenepa ni kawaida kuambiwa “FANYA MAZOEZI”, stress inakuja pale unapofanya mazoezi kwa bidii lakini haupungui.

Inawezekana ukapungua baada ya mazoezi makali, ila ukiacha tu unarudi kule kule huenda na zaidi. Matokeo yake yanakuwa sio ya kudumu.

Makosa ambayo unawezakuwa unayafanya ni kufanya mazoezi ambayo matokeo yake sio ya kudumu au unafanya mazoezi ambayo hayakusadii kupunguza uzito.

ANGALIZO:

Katika somo hili sifundishi mazoezi kwa ajili ya kupunguza tumbo. Nitafundisha kwenye somo lingine.

Kama kupunguza uzito kunahitaji upate alama 100, kuushughulisha mwili itakuchangia alama 25.

Hiyo ‘Kuushughulisha mwili’ ni pamoja na matendo yote yasiyo ya hiari kama kupumua.. kama umewahi kuwaona wagonjwa wenye shida ya kupumua kwa muda mrefu wanavyokonda.

Kwahiyo..

Jumla ya shughuli zote za hiari na zisizoza hiari zinachangia hiyo asimilia 25. Ukiondoa shughuli ambazo sio za hiari kwa sababu utazifanya utake usitake.

Zile shughuli za hiari kama kufanya kazi, kutembea, kukimbia, nk vinachangia asilimia 15.

Kama wewe ni mnene unataka kupunguza uzito inamaanisha unapambania hiyo asilimia 15 kati ya 100. Ni sehemu ndogo japo ni ya muhimu pia.

Licha ya kuwa mazoezi yanafanya sehemu ndogo ya wewe kufanikiwa bado kuna mazoezi ambayo hayakusaidii kupungua.

Kabla sijakuambia mazoezi yapi ni sahihi na yapi sio sahihi, fahamu kuwa

…”Kwa asili sisi sio viumbe wa kufanya mazoezi”… Utauliza Dr Nature unamaanisha nini..?

Kwa asili sisi sio watu wa mazoezi

MAZOEZI ninayomaanisha hapa ni ambayo unapanga kufanya kama ratiba ya mazoezi kama vile; unaamka mapema asubuhi ili ukakimbie au unapanga ratiba ya kwenda kutembea.

Kama unaamini katika UUMBAJI kama mimi utakubaliana na mimi katika hili..

Mungu alipomuumba Adam na mkewe akawapa kazi ya kufanya ‘kulima bustani na kuitunza’.. alikusudia waishughulishe miili yao kwa kazi na sio kupanga ratiba ya kukimbia.

Leo tumekuwa wastaarabu sana yaani tunalala, tunakaa, tunatembea tumekaa na kazi zetu ni za kukaa.. maisha ni full raha.

Kwa sababu hiyo..

Magonjwa yameongezeka ndio maana watalamu wakaona ili kusaidia hawa watu, tuwashauri wapange ratiba za kufanya mazoezi.

Ukitaka kuona kwamba sio asili yetu.. wewe mwenyewe mara ngapi unapanga nitaanza kufanya mazoezi kila siku. unaenda siku moja mbili au wiki unaanza kujiwekea visingizio mwenyewe..

Mara leo kuna mvua nitaenda kesho, ooh leo nina wageni au nitaanza mwezi ujao.. ahahahh ndio inakuwa imeisha hivyo.

USIJALI!… soma hadi mwisho nitakuonesha mbinu nzuri zaidi.

Mazoezi ambayo hayafai kupunguza uzito

Ukifanya haya mazoezi kama lengo lako ni kupungua unapoteza muda wako..!

Kuogelea

Ukiogelea kwa lengo la kupunguza uzito hautafanikiwa.

Tafiti zinaonesha kuwa unapofanya mazoezi kwenye maji, utakapotoka hamu ya kula na njaa inaongezeka. Utakula kufidia nishati yote uliyotumia wakati wa kuogelea.

Kufanya mazoezi gym yenye air conditioner ‘kiyoyozi’

Imekuwa vizuri gym nyingi hazina kiyoyozi.. ILA kama bado unafanya mazoezi gym au eneo lenye kiyoyozi; kama lengo lako ni kupunguza uzito unapoteza muda.

Mazoezi yatakayokusaidia kupunguza uzito

Hapa kuna aina nyingi sana za mazoezi ynayosaidia kupunguza uzito au kuzuia mtu asiwe na uzito mkubwa.

Mazoezi yoyote ambayo yatakusaidia kutoka jasho, mapigo ya moyo kwenda mbio na kutumia nguvu zaidi yanaweza kukusaidia kupata faida hii.

Mfano wa mazoezi ni kama kukimbia, kucheza michezo kama mpira, kufanya kazi ngumu; kulima, kujenga, kupanda milima, mazoezi mengine ni kama kuendesha baiskeli, kutembea na mengine kama hayo.

Sijaingia ndani kuyataja kwa sababu najua unayahamu na mengine unayafanya..

Katika mazoezi haya sio yote yatakusaidia kupunguza uzito milele YAANI.. Kupunguza uzito kwa namna ya kudumu.

Wengi wanawaweza kupunguza uzito, mziki upo kwenye kuutunza huo uzito maisha yote.

Hapa nataka nikuonesha aina ya mazoezi ambayo unaweza ukafanya yakakusaidia kupunguza uzito milele. Hiki ndio kiini cha somo hili..

Mazoezi yatakayokusaidia kupunguza uzito milele

Ukikumbuka kuwa ‘kwa asili sisi sio watu wa maoezi’ utataka kujua tufanye nini ili kuendana na asili yetu na tuweze kuishughulisha miili yetu kila siku bila kuhangaika.

Kuna mambo 3 ambayo unaweza kufanya;

... “kazi, kutembea na hobby.”

Kazi

Mungu alikusudia ili mwanadamu afya yake iwe timamu afanye kazi zinazoushughulisha mwili.

Ukifanya kazi ambazo zinaushughulisha mwili ni mazoezi tosha kabisa kwa siku. Kama kazi yako ndio mazoezi yako inamaanisha kwamba kila siku utakuwa unafanya mazoezi.

Haitakuwa ngumu kwako kwamba kupanga ratiba au kuwa na visingio vya kutokuwa na muda au hujisikii kwa sababu kinachokupa chakula ndio mazoezi yako.

Mfano wa kazi kama hizo ni; ukulima, uhandisi, ujenzi, ufundi wenye kutumia nguvu, kubeba mizigo, uaskari na namna nyingine za kazi kama hizo zinazotumia nguvu.

Hata hivyo..

Baada ya siku nzima ya kufanya kazi za kutumia nguvu, ni vizuri ukifika nyumbai kupumzika fanya mazoezi ya ku-relax kama yoga, kuvuta pumzi, massage kidogo ili ukienda kulala unajisikia kama mbinguni.

Inawezekana asili ya kazi yako haitumii nguvu ninakupendekezea anzisha bustani hapo kwako. Hata kama upo mjini kiasi gani unaweza ukaanzisha bustani ndogo.

Unapokuwa unafanya kazi kwenye bustani yako ni mazoezi mazuri sana tena yenye faida maana mwisho wa siku utakula matunda ya bustani yako.

Tembea

Kwa taarifa yako ‘kutembea ni mazoezi bora zaidi’ unayoweza kuyafanya kwa muda mrefu katika maisha yako.

Punguza ustaarabu wa kupanda gari na bajaji kila sehemu.. TEMBEAA!

Hata kama kazini kwako ni mbali au wewe ni mtu wa cheo huwezi kutembea tembea kila mahali, paki gari mbali na ofisi yako ili utembee wakati wa kuingia ofisini na wakati wa kutoka.

Tumia kila nafasi inayopatikana kutembea. Haihitaji upange ratiba inakutaka tu kuamua kutembea. kila sehemu ambayo unaona inawezekana ukajaribu kutembea, tembea. Ifanye hii iwe tabia yako.

Hii itakusaidia kuchoma mafuta na kuutunza uzito wako ukae panapotakiwa siku zote.

Hobby

Hobby ni kitu ambacho unapenda inaweza kuwa ni mchezo au burudani fulani.

Jitahidi uwe na hobby ambayo inahusiana na kutumia nguvu na kuushughulisha mwili. Kwa sababu hobby ni kitu ambacho unapenda kukifanya inamaanisha kuwa utaweza kukifanya maisha yako yote bila kuacha.

Binafsi hobby yako ni kuendesha basikeli.. napenda sana kuendesha baiskeli. kuna wakati naendesha hadi kilometa 100 narudi nimechoka sana.. lakini najisiki vizuri kwa sababu ninapenda.

Hii inanisaidia kuchoma mafuta na kuzuia nisiwe na uzito mkubwa sana kwa kuwa ni kitu ambacho nakipenda sitaacha maisha yote.

Wewe pia tafuta hobby ambayo unaipenda itakayokusaidia katika hilo kama vile kucheza mziki, kucheza mpira, kucheza sarakasi, kukimbia, kuruka kamba, kuendesha baiskeli kama mimi nk

Halafu punguza michezo ambayo inakufanya ubweteke kama video games, kamali nk.

KWA UFUPI

Ukiwa na kazi ambayo inatumia nguvu, unatumia kila nafasi inayopatikana kutembea na una hobby inakusaidia kuwa active inatosha kabisa kukusaidia kupunguza uzito milele.

Inawezekana bado unajitafuta…

Bado hauna uhakika ufanyaje lakini tayari una uzito mkubwa. Wakati huu unaweza ukatumia EASY CHOPPER

Easy chopper ni fomula ya asili ambayo inasaidia kuongeza kasi ya mwili kuchoma mafuta na hivyo inapunguza njaa za mara kwa mara na inapunguza uzito na kitambi.

“Sio chungu wala sio ya kuharisha” na Haina madhara yoyote, ni salama.

MATUMIZI

Kijiko kimoja cha dawa kwenye maji ya moto kikombe kimoja asubuhi na jioni kabla ya kula. Unatumia mpaka utakapokuwa umefikia lengo lako.

MATOKEO YA DAWA & SIDE BENEFITS

  1. Inapunguza njaa za mara kwa mara hivyo ukiona hujisikii kula au unashiba mapema ni sawa huna haja ya kula kila wakati.
  2. Inaongeza kiu ya maji utahitaji kunywa angalau lita 2 kwa siku
  3. inapunguza kilo 2 mpaka 10 kwa mwezi kulingana na lifeystyle yako.
  4. Inaongeza wingi wa choo. Kwahiyo utapata choo kingi ukianza kutumia lakini SIO YA KUHARISHA.
  5. Inatibu vidonda vya tumbo, tumbo kujaa gesi, kiungulia.
  6. Inatibu UTI sugu.
  7. Inabalance uwiano wa homoni, kama unashida ya HEDHI inasaidia. Hivyo ni rafiki kwa uzazi wa wanawake.
  8. Inaongeza HAMU ya tendo la ndoa kwa wanawake
  9. Inaongeza ufanisi wa mwanaume kwenye UNYUMBA

đŸ’° Bei ni tshs. 50,000 kwa kopo 1 ambayo ndio dozi ya mwezi 1.

Jinsi ya kupata Easy Chopper

0 0 votes
Article Rating
Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Newest
Oldest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
trackback

[…] Katika somo la ‘Mazoezi Yanayofaa na Yasiyofaa Kupunguza Uzito Milele’… […]

Share
Scroll to Top